CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),
kinatarajia kuendesha kozi ya makocha pamoja na waamuzi ili kusaidia kuinua
kiwango cha mchezo huo.
Katika kikao cha Kamati ya Ufundi, kilichoketi
Mei 11 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, chini ya Mwenyekiti wa kamati
hiyo, Joseph Kanakamfumu, alisema kozi ya ualimu wa mpira wa miguu ngazi ya
cheti (Inter-Mediate), ambayo imekuwa kwenye mahitaji makubwa, itaanza Juni 3
hadi 28 mwaka huu.
Kozi itakuwa kwa siku 10, tunatarajia kupata
washiriki watakaofikia 60, iwapo idadi hiyo itafikia na kuzidi, kutakuwa na
awamu mbili za wanafunzi ambao kisheria darasa linatakiwa kuwa na wanafunzi 35
hadi 40.
Watu wataanza kujiandikisha kuanzia
Mei 15 hadi 26 na
awamu ya kwanza ya kozi itaanza Juni 3 hadi 14 na ya pili itaanza Juni 17 hadi
28.
Kwa upande wa kozi ya waamuzi itaanza Septemba 3
hadi 9 mwaka huu na ada itakuwa Sh 25, 000.
Fomu zitapatikana katika ofisi za Mikoa ya
kisoka, TEFA, IDFA,KIFA na DRFA na kozi zote zitafanyika kwenye ukumbi huo wa
Harbours Club.
Kamati hiyo imepanga kukutana Mei 19 kwenye Ukumbi huo wa
Harbours Club saa tatu asubuhi na viongozi wote wa timu za wanawake kutathimini
michango yao kwa ukuzaji wa soka la Wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam.
Wajumbe waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya DRFA, Kennedy Mwaisabula, Jovin Ndimbo
(Mwenyekiti Kamati ya Waamuzi), Benny Kisaka (Mwenyekiti Kamati ya Soka la
Wanawake), Abdallah Mitole (Mjumbe kamati ya waamuzi), Sijali Juma (Mjumbe
kamati ya waamuzi), Richard Mbuya (Mjumbe kamati ya Soka la Wanawake) na Dk.
Maneno Tamba (Mjumbe Kamati ya Soka la Wanawake).
Imetolewa na Mohamed Mharizo
Ofisa Habari wa DRFA
No comments:
Post a Comment