Ulaji zaidi wa wadudu huenda ukasaidia dunia
kukabiliana na uhaba wa chakula, hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na
umoja wa Mataifa.
Ripoti hiyo
iliyotolewa na shirika la chakula na kilimo na UN, inasema kuwa kula wadudu
huenda kukasaidia kuboresha afya na kupunguza idadi ya watu.
Kadhalika ripoti hiyo inasema kuwa zaidi ya watu bilioni
mbili duniani hula wadudu kama sehemu ya lishe
bora.
Hata hivyo inasema kukerwa kwa watu na kuwaona
wadudu ndicho kinasalia kuwa kikwazo kikubwa katika nchi nyingi za Magharibi.
Nyingu
au (Wasp), Beetle pamoja na wadudu wengine, hawatumiki sana
kama chakula kwa binadamu au wanyama,
kulingana na ripoti hiyo.
Kilimo
cha kufuga Wadudu ni moja ya njia za kusuluhisha tatizo la uhaba wa chakula
"wadudu
wako kila mahali, na kuzaana kwa haraka, na pia hukuwa kwa haraka sana pamoja
na kuwa na athari ndogo sana kwa mazingira,'' ilisema ripoti hiyo.
Thamani
ya wadudu kwa afya.
Waandishi
wa ripoti hiyo wamesema kuwa, wadudu wanaleta afya nzuri , wakiwa na viwango
vya juu vya Proteni , mafuta na madini mengine.
''Wana
umuhimu mkubwa kwa kuwa na uwezo wa kuongeza madini mwilini, hasa kwa watoto
wenye utapia mlo.''
Wadudu
pia ni muhimu sana
kwa sababu wanakula chakula kidogo kuliko wanyama. Mfano Chenene (cricket)
wanakula chakula kidogo sana
ikilinganishwa na mifugo ingawa wana viwango sawa vya madini ya Proteni.
Aidha
wadudu hao pia wana athari ndogo sana
katika uchafuzi wa mazingira ikilinganishwa na mifugo.
Gesi
aina ya Ammonia inayotolewa na wadudu kadhaa, ni ya chini mno ikilinganishwa na
ile inayotolewa na mifugo mfano Nguruwe.
Ripoti hiyo inataka
mikahawa kuwa na wadudu miongoni mwa vyakula wanavyouza.
Wadudu
huliwa na watu wengi duniani lakini dhana hiyo haiwezi kufanikishwa kwa watu wa
nchi za Magharibi.
Ripoti
hiyo inapendekeza kuwa sekta ya chakula inaweza kusaidia katika kuhamasisha
watu kubadili wanavyokula na hata kuonyesha watu kuwa wanaweza kula baadhi ya
vyakula.
Katika
sehemu kadhaa duniani wadudu kadhaa huonekana kama
chakula kitamu.
Mfano
Viwavi huliwa Kusini mwa Afrika na huonekana kama
chakula cha hadhi ya juu na pia huuzwa kwa bei ghali.
Wadudu
wengi wanaoliwa hutolewa msituni na hutumiwa na watu maalum.
Ripoti
hiyo Inapendekeza kuwepo sheria ya kudhibiti uzalishaji wa wadudu kama chakula.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment