Dar es Salaam/Arusha. Serikali za Saudi Arabia
na Falme za Kiarabu (UAE) zimezungumzia kukamatwa kwa raia wake, ambao
wanahusishwa na tuhuma za kurushwa kwa bomu kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu
Joseph Mfanyakazi, Arusha, Jumapili iliyopita.
Watu watatu walifariki dunia na wengine
60, akiwamo Balozi wa Vatican nchini na Mwakilishi wa Papa, Francisco
Montecillo Padilla wakijeruhiwa baada ya bomu kurushwa wakati wa ufunguzi wa
kanisa hilo
lililoko Parokia ya Olasiti.
Watu tisa wamekamatwa kuhusiana na tukiohilo la
kigaidi, kati yao
Watanzania ni watano na raia wageni wanne.
Watu tisa wamekamatwa kuhusiana na tukio
Viongozi wa Serikali walikaririwa
wakisema wageni waliokamatwa raia watatu ni wa Saudi Arabia na mmoja wa UAE ambao
walikamatwa wakati wakiondoka nchini kupitia Namanga.
Balozi wa Saudi Arabia
Balozi wa Saudi Arabia nchini, Hani Momina alikaririwa na mashirika ya habari ya kimataifa akikiri kukamatwa kwa raia wa nchi yake na kusisitiza kwamba hakukuwa na ushahidi wa kumhusisha na shambulizi hilo kwani alikuja Tanzania kutalii.
Balozi wa Saudi Arabia
Balozi wa Saudi Arabia nchini, Hani Momina alikaririwa na mashirika ya habari ya kimataifa akikiri kukamatwa kwa raia wa nchi yake na kusisitiza kwamba hakukuwa na ushahidi wa kumhusisha na shambulizi hilo kwani alikuja Tanzania kutalii.
Momina alisema alikutana na Mwenyekiti
wa Kikosi Kazi kinachochunguza suala hilo kwenye
kituo cha polisi anaposhikiwa raia wake akitaka kujua kama
mtu wao amewekwa vizuri.
“Tuna matumaini makubwa kuwa wataachiwa na tutaendelea kufuatilia suala lao hadi tuone mwisho wake,” alisema Balozi huyo na kusisitiza kwamba hawaondoki Arusha.
“Tuna matumaini makubwa kuwa wataachiwa na tutaendelea kufuatilia suala lao hadi tuone mwisho wake,” alisema Balozi huyo na kusisitiza kwamba hawaondoki Arusha.
Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya UAE, kupitia mtandao wa
Twitter ilieleza kuwa inafuatilia kwa karibu suala la raia wake watatu
waliokamatwa. Ilisema walikuwa wanafanya kazi kwa karibu na ubalozi wa nchi yao huko Tanzania
ili kufahamu hatima ya watu wao.
UAE imesema inapinga kwa nguvu zote vitendo vya ugaidi na iko
tayari kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania
juu ya raia wake kuhusishwa na tukio hilo .
Majeruhi saba waletwa Dar
Majeruhi saba wa mlipuko huo walisafirishwa kwa ndege kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya hali zao kuwa mbaya.
Majeruhi saba wa mlipuko huo walisafirishwa kwa ndege kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya hali zao kuwa mbaya.
Majeruhi waliosafirishwa jana ni Jenipha Joachim aliyeumia
kwenye mapafu na miguuni. Alimpoteza mtoto wake, Patricia Joachim juzi.
Wengine ni Fatuma Tarimo, ambaye chembechembe za vyuma zimeingia
tumboni, Apolinary Malasha aliyejeruhiwa miguu na jicho kutokana na masalia ya
vyuma vya mabomu, Albert Njau ambaye amedhurika mbavu na mgongo na Faustin
Shirima ambaye amekutwa na vyuma tumboni.
Wengine ni Gabriel Godfrey (9) ambaye ana chembechembe za bomu
tumboni na miguuni na Athanas Mrema(14) ambaye amevunjika mbavu na pia ana
chembechembe za vyuma tumboni.
Kutokana na tukio hilo , wabunge
walichangia posho yao
kwa kikao cha jana ambayo ni Sh200,000 kwa kila mmoja.
Utata aliyefariki KCMC
Jina la mtoto Patricia Assey (9) ambaye ni miongoni mwa waliouawa katika mlipuko wa bomuhilo
lilizua utata jana kiasi cha kufanya uongozi wa Hospitali ya KCMC na polisi
kuzuia mwili wake kwa muda.
Jina la mtoto Patricia Assey (9) ambaye ni miongoni mwa waliouawa katika mlipuko wa bomu
Wakati huo huo taarifa za jana zinaeleza
kuwa majeruhi wameanza kutoa ya moyoni kuhusu kilichotokea na kueleza kuwa Bomu
lililorushwa na kuua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60 kwenye Kanisa
Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi huko Arusha, inadaiwa lilitengenezwa
kienyeji.
Wakati kukiwa na madai hayo, mazishi ya marehemu hao Regina
Kurusei, (45), James Gabriel (16) na Patricia Joachim (9) yanatazamiwa kufanyika
leo Olasiti, Arusha na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anatarajiwa kuhudhuria.
Ofisa mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye
hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alimdokeza mwandishi wetu jana kuwa kwa
ujuzi na uzoefu wake wa masuala hayo, bomu hilo si la kiwandani akisema msingi
wa imani yake ni jinsi vyuma vilivyotawanyika na kuumiza watu zaidi ya 20.
Watu saba wamefikishwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kwa ajili ya kuondolewa vyuma na kupata matibabu zaidi.
Mstaafu huyo alieleza kuwa mabomu mengi zaidi ya kienyeji
hutengenezwa kwa kutumia bakuli za chuma, zikiwekewa baruti ndani na kufungwa
kwa waya.
“Hawa jamaa huweka vipande kama 36 vya baruti na hufungiwa ndani
ya bakuli kwa kubanwa sana ili kuvipa joto na
bomu likitua, husababisha madhara makubwa,” alisema ofisa huyo ambaye
alishiriki Vita ya Uganda
mwaka 1978 hadi 1979.
Mstaafu huyo alisema mabomu ya aina hiyo yametumika kwenye
mashambulizi ya kigaidi katika nchi mbalimbali duniani kama Lebanon , Vietnam ,
Libya , Ireland Kaskazini ,
Syria , Afghanistan , Iraq ,
Chechnya na India .
Mmoja wa majeruhi, Mwalimu Fatuma Tarimo amesimulia
alivyoshuhudia bomu likitua mbele yake na kulipuka.
Tarimo, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
alisema jana kuwa aliliona bomu hilo likiwa na
rangi ya shaba .
Pia alisema lilikuwa na waya kwa juu.
“Baada ya kutua, nilisikia kishindo kikubwa nikashtuka ikabidi
niangalie. Baada ya kuona ni kitu kama chuma
nilipata hofu nikafikiria kuondoka,” alisema mwalimu huyo wa Shule ya Msingi ya
Burka Estate, nje kidogo ya Jiji la Arusha. Hata hivyo, alisema kabla ya
kuondoka, alishtukia amenyanyuliwa juu na hakujua kilichoendelea kwani
aliposhtuka alijikuta akiwa katika Hospitali ya Mount Meru .
Tarimo ametolewa kipande cha chuma
katika mguu wake wa kulia.
“Nina maumivu bado lakini nina matumaini nimechukuliwa kipimo cha ‘T-Scan’ kwa matibabu zaidi,” alisema Mwalimu Tarimo ambaye anaaminika kuwa na kipande kingine kwenye mapafu.
“Nina maumivu bado lakini nina matumaini nimechukuliwa kipimo cha ‘T-Scan’ kwa matibabu zaidi,” alisema Mwalimu Tarimo ambaye anaaminika kuwa na kipande kingine kwenye mapafu.
Majeruhi mwingine, Jenipher Joackim
ambaye amefiwa na mwanaye Patricia Joackim (9) hana taarifa za kifo hicho
kilichotokea katika Hospitali ya KCMC.
“Nimeambiwa kwamba yupo ICU sijui anaendeleaje,” alisema.
“Nimeambiwa kwamba yupo ICU sijui anaendeleaje,” alisema.
No comments:
Post a Comment