Sunday, July 22, 2012

Futari ya leo...

Ndugu zangu,

Leo wapo waliofikisha siku ya pili katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, na wapo waliofikisha siku ya tatu. Kimsingi wote ni waislamu na nia yao ni moja, kupata fadhila za Muumba wa ardhi na mbingu. Ibada ndiyo itamtofautisha mmbora katika viumbe mbele ya Mwenyezi Mungu.

Leo nitawaletea futari ambayo kama nilivyotangulia jana, itakufanya upate afya na si maradhi. Kwa maana watu wengi hawajui kutofautisha faida ya vyakula na mwili. Kwa maana wengi hukimbilia utamu ama ladha nzuri ya chakula kuliko faida yake kiafya.

Futari yetu tutapika Viazi vitamu (sweet potatoes) vinaweza kuwa vya karanga, nazi ama vya kuchemsha. Halafu tunapika na maandazi (maamri), tutapika na makaroni, mchuzi wa mayai yaliyokaangwa pamoja na nyanya, vitunguu na pilipili hoho ama (green paper). Halafu na mchuzi wa nyama ya kuku, (pendelea sana kula nyama nyeupe (white meet) kuliko nyama nyekundu (red meet).

Baada ya hapo pata tunda aina ya tufaa (apple) na tende ambazo hazijaiva sana. Matunda kama nilivyosema jana zile nyuzinyuzi (fiber) husaidia mmengenyo (digestion) wa chakula. Halafu tengeneza chai ya mkandaa (black tea) ambayo utachanganya na pilipili manga (black paper) ama tangawizi (ginger), ambayo itasaidia kuongeza ladha na hamu ya kula. Usisahau kunywa maji mengi.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894, 0752 593894
22/07/2012
hafidhkido@yahoo.com  

No comments:

Post a Comment