Anton Ferdinand
ameieleza mahakama siku ya Jumatatu kwamba 'ningelikerwa sana '
na matamshi ya ubaguzi wa rangi kama
ningelimsikia John Terry akitamka maneno hayo.
John Terry, mwenye umri
wa miaka 31, na ambaye ni mchezaji soka wa Chelsea
na vile vile timu ya taifa ya England ,
anashtakiwa kwa madai kwamba alimtukana Anton Ferdinand, kwa kutumia lugha ya
ubaguzi wa rangi katika mechi uwanjani, madai ambayo John Terry ameyakanusha.
Inadaiwa Terry, nahodha
wa timu ya Chelsea, alitamka maneno hayo dhidi ya mlinzi wa QPR, wakati timu
hizo zilipopambana katika uwanja wa QPR wa barabara ya Loftus, mwezi Oktoba.
Kesi hiyo inatazamiwa
itaendelea kwa siku tano katika mahakama ya Westminster ,
mjini London .
Ikiwa Terry atapatikana
na hatia, hukumu kali zaidi itakuwa ni kutozwa faini ya pauni 2,500.
Ferdinand alisema
mahakamani kwamba "wakati mtu anapoleta suala la rangi katika mchezo, huwa
amezidisha matusi na kuyafikisha hatua nyingine".
Inadaiwa kwamba mlinzi
huyo wa Chelsea
alimuita mwenzake mweusi, na akitumia maneno pia yaliyohusishwa na ngono.
Mtaalamu wa lugha ya
kutafsiri yaliyosema kwa kuangalia mdomo, Susan Whitewood, alithibitisha kwamba
matamshi yasiyofaa yalitumiwa na Terry.
Ferdinand aliielezea
mahakama kwamba awali hakudhani lugha ya ubaguzi wa rangi ilitumika.
Lakini baada ya mechi,
rafiki yake wa kike alimchezea video iliyokuwa katika tovuti ya YouTube, na
baada ya hapo, alibadilisha nia na kuamua kuchukua hatua za kisheria.
Ferdinand alisema kwamba
kama moja kwa moja angelitambua Terry
alimtukana uwanjani kwa kutumia matamshi hayo, basi papo hapo angeliwaarifu
maafisa waliyosimamia mechi hiyo.

No comments:
Post a Comment