Meli ya kisasa karibuni kuzinduliwa inauwezo
kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.
KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia
kuzindua meli kubwa ya kisasa kwa ajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja.
Meneja
Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo
yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa. Mohamedi alisema shida ya usafiri
itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba
abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda
na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.
Waziri
Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo
ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na
siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20

No comments:
Post a Comment