Leo nimekerwa sana na hawa makarani wa vitambulisho vya taifa/ukaazi. Maana mwenyewe leo nimekaa nyumbani ndiyo nafasi yangu kuenda kujiandikisha. Nikakusanya kila kilichohitajika badala yake nikaambiwa zoezi la leo ni la kuzungumza na waliokwishajiandikisha na sisi ambao bado turuji jumatatu. Sasa ikiwa mtu unakwenda ofisini jumatatu mpaka ijumaa tutapata wasaa wa kujiandikisha kweli?
Huyu ni mtumiaji wa dawa za kulevya, anaitwa 'Pachanga' jina la utani. Watu kama hawa ni nadra sana kuitikia wito wa kujiandikisha mambo ya msingi kama haya. Na yeye pia ameambiwa aje jumatatu, atarudi kweli?
Hivi ndivyo vifaa nilivyokusanya ili kuweza kujiandikisha, lakini jembe pia nimedunda. Utadhani nilikuwa naomba viza ya kusafiria.....
No comments:
Post a Comment