Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewanasihi Wananchi kuendelea kuiamini
Serikali katika kupokea Taarifa zake hasa wakati wa kutokea Majanga na Maafa.
Nasaha hizo
amezito hapo katika Ofisini yake iliyopo Baraza la Wawakilishi Mbweni nje
kidogo ya Mji wa Zanzibar
wakati akipokewa mkono wa Pole kutoka kwa Taasisi mbali mbali za Umma na
Kijamii.
Salamu hizo za
mkono wa pole zimetolewa kwa Balozi Seif na Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii Zanzibar { ZSSF } na ule wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii ya Tanzania { NSSF
} ambapo kila moja ilikabidhi mchango wa Shilingi Milioni kumi { 1,000,000/-
}.
Balozi Seif
alisema Jamii kujenga tabia ya kuiamini Serikali hupelekea kuwepuka
kuchanganywa wakati wa kupokea Taarifa hizo kutoka vyombo vya Habari
vinavyopokea Baadhi ya Taarifa zisizo rasmi.
Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa mifuko
hiyo ya Hifadhi ya Jamii Bara na Zanzibar kwa
kufikiria jambo hilo
muhimu la kutoa mchango ambalo Taifa linahitaji kuungwa mkono katika
kukabiliana nalo.
Aliuhakikishia
Uongozi wa Taasisi hizo kwamba michango hiyo itasimamiwa vyema kwa ajili ya kuwafika
waliohusika kwa kutumia utaratibu uliotumika wakati wa ajali iliyotokea Mwaka
jana.
Alisema licha ya
zoezi la uokozi kuwa na gharama kubwa lakini Serikali inaendelea kutoa huduma
zote za mazishi na usafirishaji wa maiti zinazopelekwa Tanzania Bara ambazo
zilipatikana kutokana na ajali ya Meli ya M.V Skagit hapo juzi.
Aliongeza kuwa
shughuli hiyo ikiwemo gharama za vyombo, mafuta, Chakula na uokozi zinahitaji
kuungwa mkono na taasisi na jumuiya ya kiraia ndani na nje ya Nchi. “ Serikali
imeshachukua jukumu la kuzizika zile Maiti zilizoshindwa kutambulika hadi sasa,
kuzisafirisha maiti tatu hadi Tanzania Bara pamoja na familia nne wakati maiti
moja ya raia wa kigeni bado haijatambulika”. Alifafanua Balozi Seif.
Alisisitiza
kwamba katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo
wazamiaji wa Israel
walioko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja wameamua kusaidia kazi ya uokozi kwenya
Meli hiyo ili kuendelea kutafuta miili ya Watu iliyopotea.
Mapema
Meneja Msuluhishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } Ndugu Khamis
Phil Phil Than alisema yapo mambo mengi kwenye tukio hilo la Maafa ambayo yanahitajika kupata
msukumo kutoka kwa Washirika, Taasisi na Jumuiya za Kiraia. Ndugu Phil Phil
alisema mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar umekuwa mstari wa mbele katika
kutekeleza majukumu yake yaliyolenga zaidi kwenye eneo la Jamii.
Naye
kwa upande wake Ofisa Muandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Tanzania { NSSF } kutoka Makao Makuu Mjini Dar
es salaam Nd. Juma Kimtu alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Taasisi hiyo imeamua kutoa
mchango huo baada ya kuona uzito Maafa yaliyotokea ambayo yameigusa Jamii yote.
Ndugu
Kimtu alisema Serikali kwa kuwa ni ya watu haina budi wakati wote kusaidiwa
hasa katika masuala ya Majanga na Maafa ambayo kwa kiasi kikubwa huigusa Jamii
yote.
Na
Othman Hamisi Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili Wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment