Hiki ni kitabu kabambe, bado ni kipya na watu wachache sana wanacho. Mhariri
wangu jana alinionyesha na nikabahatika kukigusa na kupiga nacho picha.
Naam ushamba unasaidia kujua mambo, nilishawahi kuwauliza
wadau katika ukurasa wangu wa facebook ikiwa kuna atakaebahatika kukipata
kitabu hiki anijulishe.
Kifupi mwandishi Andrew Feinstein, amefanikiwa kuelezea
namna wizi wa fedha za umma ambazo baadae zilihusika kununulia rada ya kijeshi.
Katika kitabu hiki cha The Shadow World, Inside the Global
Arm Trade: kinachambua namna aliekuwa Gavana wa Bank Kuu ya Tanzania (BOT)
wakati huo Dr Idrisa Rashid na aliekuwa mwanasheria mkuu wa Serikali Andrew
Chenge, waliiibia serikali mamilioni ya pesa wakisaidiana na watanzania wawili
wenye asili ya kiasia Tanil Somaiya mmiliki wa kampuni ya uwakala wa simu ya
shivacom na Sailesh Vithlan.
Mchakato wa wizi huo wa zaidi ya dola za kimarekani mil 40 ulianzia
mwaka 1997 wakati wa kipindi cha Mzee Mkapa, na kupitia Bank ya Barclays
walifanikiwa kupata mkopo wa mamilioni ya pesa na kununua rada hiyo kwa bei
chee kutoka kampuni ya kuuza silaha ya Uingereza iitwayo BAE System. Mbali na
upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya wabunge na mawaziri katika bunge la
Uingereza kupinga nchi masikini kununua rada ya kijeshi wakati haina hata ndege
za kisasa za kivita.
Tafadhali subiri kusambaa kwa kitabu hicho ujisomee
mwenyewe, hata mimi jembe lenu nimeshindwa kununua maana hakijaingia rasmi
kinapatikana kwa uchache sana .
HAFIDH KIDO
0752 593894/ 0713 593894
DAR ES SALAAM ,
TANZANIA
No comments:
Post a Comment