Tuesday, July 10, 2012



Ndugu zangu

Jana nilikutana na kichekesho cha mwaka, ni mambo ambayo nilizoea kuyaona nikiwa nchi jirani ya Uganda; uzembe katika biashara.

Nilikuwa nataka kutoa pesa katika simu (tigo pesa), katika akiba yangu nilikuwa na shilingi elf 5 tu za kitanzania, na nikatakiwa kutoa shilingi elf 4. Ubaya ukaja kwenye kukubaliwa kupata hiyo pesa, mhudumu katika kibanda cha tigo pesa alinambia hivi.

"Siwezi kutoa hiyo pesa (4000), maana sina chenji, kama ungetoa elf 5 ingekuwa vizuri." nikamuuliza kwanini huendi kuomba chenji ya hiyo elf 5 unipatie elf 4? akanijibu "Hapana sina huomuda unaweza kuenda tu."

Kaazi kwelikweli, sidhani kama tunaweza kufika tulipopakusudia.

HAFIDH KIDO

0713 593894/ 0752 593894
DAR ES SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment