Ndugu zangu
Juzi niliangalia taarifa ya habari nikaona nmna nchi ya Marekani inavyojua namna ya kucheza na akili za watu kwa kutumia misaada. Ilionyeshwa namna Waziri wa masuala ya nje Hillary Clinton, alivyofanya ziara ya kushtukiza nchini Afganistan kwa madai walitaka kuitangaza nchi hiyo moja ya washirika wakuu wa Marekani.
Alionyeshwa namna Rais wa Afganistan Hamid Karzai, alivyoonyesha kufurahishwa na uamuzi huo hasa wa kitendo cha Hillary Clinton kuacha shughuli zake na kuja katika ghafla hiyo. Kuna mambo mengi ambayo ubongo wangu wa nyuma unayafikiri kwa kipindi hiki lakini sitaki kuzungumza yote ni mapema mno.
Kipo kinachotafutwa katika nchi hiyo lakini turidhike tu kuwa nchi ya Marekani haina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu. Maana kumbukumbu zangu zinaniambia nchi hiyo hiyo ya Marekani ilikuwa na urafiki mkubwa na nchi ya Iraq wakati wa Sadam Hussein, baadae wakawa maadui wakubwa wa Iraq, na sasa kila siku wanatangaza kuondoa majeshi yao katika nchi hiyo lakini bado wanaikalia kimabavu.
Lipo litakalofuata baada ya urafiki huu wa mashaka baina ya Afganistan na Marekani, maana wana historia ndefu tangu kuwa vitani wakidai kuitetea wakati Warusi walipokuwa na urafiki na Waafganistan, akatumika Osama Bin Laden na Mulah Omar kuwaondoa Warusi.
Baadae Wamarekani wakajenga uadui mkubwa na nchi hiyo baada ya kumkumbatia Osama, lakini walipoona Osama ameondoka duniani kimaajabu sasa wameamua kurudi. Tusubiri.
HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894, 0752 593894
No comments:
Post a Comment