Sunday, July 22, 2012

Ndugu zangu, leo nimeamka na udobi. Namshukuru Mungu nimefua nguo za kutosha. Hata shuka langu leo limebahatika kuonja maji, nadhani huu ni wakati muafaka wa kupata mwenza wa ubani tusaidiane shughuli kama hizi. Ila nimefurahishwa na majembe yangu mawili yamenisaidia kufagia ua....


 Majembe yangu mawili haya niliwaambia ni wakakamavu kama baba yao, na hapo wamedhihirisha kwa kunisaidia kufagia. Wa kushoto ni Athumani na wa kulia ni Hafidh jr. Leo asubuhi....

 Leo hata shuka langu limebahatika kuonja maji baada ya kukaa bila ya kufuliwa kwa miezi kadhaa... Umeliona lipo ndani ya ndoo?

Majembe haya yakigombania kutupa taka ndani ya ndoo, hili ndilo tatizo lao kila mtu anataka kuonekana mkakamavu mbele ya baba yake.

No comments:

Post a Comment