Marekani imekata msaada wa
kijeshi inayoipa Rwanda ,
huku kukiwa na wasiwasi kuwa Rwanda
inawasaidia katika mapigano yanayoendelea nchi ya jirani, yaani Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo .
Wizara ya Ulinzi imesema itazuwia dola 200,000
zilizokusudiwa kulisaidia jeshi la Rwanda .
Msaada
wenyewe uliokatwa siyo mkubwa kwa jeshi la Rwanda , lakini hatua hiyo inatoa
ishara kubwa.
Marekakni
inaitetea sana Rwanda katika jumuia ya kimataifa.
Kwa
kukata msaada huo, Marekani ni kama inasema "tunaamini ripoti kuwa Rwanda inatibua usalama wa kanda hiyo kwa
kuwaunga mkono wapiganaji wa Congo ".
Mwezi
uliopita, Umoja wa Mataifa ulikabidhi ripoti kwa Baraza la Usalama, ambayo
ilisema ina ushahidi mzito kuwa Rwanda
inalipatia kundi la M23, wapiganaji na zana, na kurahisisha makamanda wao
wakubwa kusafiri na kuvuka mpaka baina ya Congo
na Rwanda .
Uasi
huo ulianza mwezi wa Aprili, wakati wanajeshi mia kadha wa jeshi la Congo
walipofanya ghasia.
Uasi
huo uliongozwa na Jenerali Bosco Ntaganda, ambaye anasakwa na Mahakama ya Jinai
ya Kimataifa, ICC, kwa uhalifu wa vitani.
No comments:
Post a Comment