JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA MABADILIKO YA
KATIBA
___________
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
___________
Kufuatia Ajali ya Meli
Zanzibar, Tume ya Mabadiliko ya Katiba Yasitisha Mikutano ya Kukusanya Maoni
Kusini Pemba
Alhamisi, Julai 19, 2012
Tume ya Mabadiliko ya
Katiba imepokea kwa masikitiko makubwa Taarifa ya ajali ya Meli ya MV SKAGIT
iliyotokea jana, Jumatano, tarehe 18, Julai 2012 katika eneo la Chumbe, Zanzibar .
Kutokana na msiba huu
mkubwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatoa Taarifa kwa Wananchi kuwa imesitisha
Mikutano ya kukusanya Maoni ya Wananchi kuhusu Katiba Mpya iliyokuwa inaendelea
katika Mkoa wa Kusini Pemba. Mikutano iliyositishwa ni ile iliyopangwa kufanyika
kuanzia leo, Alhamisi, Julai 19, 2012 hadi Jumamosi, Julai 21, 2012 katika
maeneo ya Wawi, Vitongoji, Chanjamjawiri, Pujini, Gombani na Wara.
Zoezi la kukusanya Maoni
litaendelea kuanzia Jumapili tarehe 22, Julai, 2012. Ratiba ya Mikutano katika
maeneo yaliyositishwa itatolewa baadaye.
Tume ya Mabadilikio ya
Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa mabadiliko haya hayahusu mikutano
ya kukusanya maoni inayoendelea kufanyika katika mikoa sita (6) ya Tanzania
Bara ambayo ni Pwani, Tanga, Dodoma ,
Shinyanga, Kagera na Manyara. Tume inawaomba wananchi wa Mikoa hii kujitokeza
kwa wingi na kutoa maoni yao .
Mwisho, Tume ya
Mabadiliko ya Katiba inatoa pole kwa wafiwa, majeruhi na wote walioguswa na
ajali hii na tunamuomba Mwenye Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema
peponi na majeruhi wote wapone kwa haraka.
Imetolewa na:
Tume ya Mabadiliko ya
Katiba,
S.L.P. 1681,
DAR ES SALAAM,
Simu: 2137833,
Simu ya Mkononi: 0757
500800
No comments:
Post a Comment