Kundi la wazee kutoka nchini Kenya
wanaodai kuwa walinyanyaswa na kuteswa na utawala wa kikoloni wa Uingereza
takriban miaka hamsini iliyopita wamewasilisha kesi yao
mjini London .
Mwaka mmoja uliopita Mahakama iliamuru kuwa
Serikali ya Uingereza haiwezi kujibu tuhuma za vitendo vya watumishi wa Mamlaka
ya ukoloni.
Wapiganaji
hao ambao wanadai kunyanyaswa na serikali ya kikoloni wakati wakipigania uhuru
wa Kenya
kutoka kwa Uingereza.
Wazee
hao walikuwa wapiganaji wa kundi la Maumau ambalo lilishiriki harakati za uhuru
wa Kenya
zaidi ya miaka hamsini iliyopita wanasema waliteswa.
Wanadai kuwa maafisa wa Kikoloni wa Uingereza
waliwatendea vitendo vya kinyama ikiwemo kuzuiliwa katika
kambi,kupigwa,kudhalilishwa kijinsia na hata baadhi ya wanaume kufinywa sehemu
zao za siri.
Yote hayo wanasema ni kwa sababu walipinga utawala wa kikoloni.
Yote hayo wanasema ni kwa sababu walipinga utawala wa kikoloni.
Sasa
wanataka serikali ya Uingereza iwalipe fidia kutokana na mateso hayo. Mawakili
wanaowakilisha kundi hilo wanasema wateja wao ni
sehemu ndogo ya mamia ya washiriki walio hai kwa sasa nchini Kenya ambao walipitia mateso kama
hayo. Wenzao wengine walifariki katika miaka iliyopita.
Awali serikali ya Uingereza ilikuwa imesema
haiwezi kuchukua lawama kwa vitendo vilivyotendwa na a utawala wa kikoloni kati
ya mwaka 1950 na 1960.
Hata
hivyo mwaka jana Jaji wa mahakama kuu mjini London akatoa uamuzi kuwa kesi ya wapiganaji
hao wa zamani ina msingi na inapaswa kusikilizwa.
Sasa
wapiganaji hao watapata fursa ya kutoa ushahidi wao mahakamani kupitia wenzao
Ndiku Mutua, Paulo Nzili, Wambugu wa Nyingi na mwanamke pekee Jane Mara wote
ambao wamefika hapa London
kwa shughuli hiyo.
Serikali
ya Kenya
imeahidi kulipa gharama ya kuendesha Kesi hiyo.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment