Tuesday, August 7, 2012

Azama wamepata kocha mpya kutoka Serbia...


Boris Bunjak kocha mkuu mpya wa timu ya Azam FC akipiga picha wakati alipotambulishwa rasmi na uongozi wa timu hiyo leo jijini Dar es salaam.

Boris Bunjak raia wa Serbia aliyezaliwa mwaka 1954 amesaini mkataba wa kuitukimia Azam FC kwa muda wa miaka miwili akiiitumikia timu hiyo, Bunjak amefundisha timu mbalimbali katika nchi za kiarabu na amewahi kuchezea timu ya taifa ya Serbia na vilabu mbalimbali huko Ulaya Mashariki amewahi kufanya kazi pia katika chama cha soka cha Yugoslavia mwaka 1993-1994 na kazi nyingine nyingi kuhusiana na masuala ya soka.

Kocha huyo amekuja kuchukua nafasi ya kocha ya Stewart Hall mwingereza alietupiwa viragona timu hiyo wiki iliyopita baada ya kumalizika kwa michuano ya Kagame.

No comments:

Post a Comment