Ecuador imeamua kumpatia hati ya ukimbizi muasisi wa
mtandao wenye utata wa Wikileaks, Julian Assange.
Ubalozi wa Ecuador
mjini London
umesema kuna wasi wasi kuwa haki za kibinadam za Bwana Assange huenda huenda
zikakiukwa.
Assange amekuwa akiishi kwenye ubalozi wa
Equador mjini London kwa miezi miwili iliyopita
kuepuka kupelekwa nchini Sweden
ambako anakabiliwa na mashtaka ya ubakaji.
Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imesema
uamuzi wa Bwana Asange wa kuomba hifadhi ya ukimbizi hautahujumu azma na nia yake
ya kutaka asafirishwe hadi nchini Sweden , kufunguliwa mashtaka.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Equador,
Ricardo Patino, amesema kuna hatari kuwa Bwana Assange akasafirishwa kutoka
Swesen kwa lazima hadi Marekani, kukabiliana na mashtaka ya kufichuliwa kwa
mtandao wake wa kidiplomasia.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ecuadorean,
Ricardo PatiƱo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa nchi yake itachukua hatua
ziwezekanazo kukwepa kile akilichokitaja kuwa ni uvunjaji wa sheria za
kimataifa.
Serikali ya Uingereza imesema, haitamruhusu
Bwana Assange, kuondoka nje ya ubalozi huo na kuwa atakamatwa atakapotoka nje.
Akitangaza uamuzi wa serikali yake Bwana
Platino amesema, Ecuador
inaamini madai yaliyotolewa na Bwana Assange kuwa ananyanyaswa kisiasa ni ya
kweli.
Tangazo hilo
lilitolewa moja kwa moja njia ya video kutoka mji mkuu wa Ecuador , Quito .
Nje ya ubalozi wa Ecuador ,
mjini London , wafuasi wa Bwana Assange ambao
walikuwa wamekusanyika walifurahiswa na tangazo hilo .
Mwandishi wa masuala ya kisheria wa
BBC, Clive Coleman amesema uhusiano kati ya Uingereza na Ecuador umehujumiwa pakubwa na uamuzi huo wa
kuumpa hifadhi bwana Assange na hatma ya ubalozi huo mjini London haijulikani.
Chanzo: BBC Swahili
<
No comments:
Post a Comment