Koffi Olomide, ambaye ni mwanamuziki mashuhuri barani
Afrika ameshitakiwa kwa kumpiga Mtayarishaji wake wa muziki.
Mwanamuziki huyo alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha
polisi na kufikishwa mahakamani jumatano.
Koffi alikamatwa kufuatia vurugu katika hoteli
moja mjini Kinshasa .
Waandishi
wa habari wanasema mahakama hiyo ya Kinishasa ilifurika kutokana na watu wengi
kuja kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi
hiyo iliharishwa hadi Alhamisi asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.
Wakati
wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide aliwakilishwa na mawakili 10.
Ugomvi
kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu
pesa dola $3,680.
Hakimu
alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela
miezi sita.
Olomide
ni gwiji wa muziki aina ya "soukous", mtindo ulitokana na jina la
kifaransa "secouer", lenye maana ya kujitikisa au kujinengua ,na
wachezaji wake vile vile wanatambulika kwa kunengua maungo.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment