Thursday, August 16, 2012

Futari ya leo

Asalam Allaykum,

Ramadhani inakwenda zake hiyo, zimebaki siku mbili tu kuimaliza. Hivyo ni vema hata katika futari zetu tusile vitu vingii bali tuwe tunakula kidogo ili kuyazoesha matumbo kuanza kula mchana.

Futari yetu ya leo itakuwa ni chips na kuku ama samaki wa kukaanga. Unaweza kupata kikombe cha uji kabla ya futari yako ukila na tende mbivu ili kuweka sawa tumbo halafu unakula chips na soda ama juice.

No comments:

Post a Comment