Bunge la zamani...
Bunge la Kenya lililokarabatiwa na ambalo limekuwa gumzo
kubwa kwa sababu ya gharama ya viti vya bunge hilo, hatimaye limefunguliwa
rasmi na rais wa nchi hiyo Mwai Kibaki.
Viti
hivyo vimegharimu dola 3,000 za kimarekani kwa kila kiti kimoja vikiwa jumla ya
350 vimetengenezwa na kitengo cha magereza nchini humo.
Zabuni
ya kwanza ya kutengeneza viti hivyo ilitolewa kwa kampuni moja ya nje lakini
ilifutwa baada ya baadhi ya wabunge kugundua kila kiti kingegharimu dola 5000
za kimarekani.
Maafisa
wanasema ukarabati huo uliogharimu dola milioni 12 utaliweka bunge katika mfumo
mpya wa kisasa wa komputa.
"Mabadiliko
tunayoyafanya yataleta mabadiliko chanya katika uongozi," spika wa bunge
Kenneth Marende ameiambia BBC.
Amesema
mfumo wa kupiga kura wa elektroniki utawawezesha wabunge kupiga kura kwa uhuru
wao binafsi kuliko kulazimika kupiga kura kwa kuhofia vyama vyao.
"sasa
mbunge atakuwa peke yake, huru kabisa binafsi, atafanya maamuzi yake na
kubonyeza tu kitufe."
Mwandishi
wa BBC Odeo Sirari mjini Nairobi , anasema baadhi
wanaona viti hivyo kuwa ni vya gharama kubwa sana kuliko mabunge mengine katika jumuiya ya
madola.
Waziri
mkuu wa Kenya Raila Odinga
na rais Mwai Kibaki pamoja na wabunge ni miongoni mwa wanaolipwa mshahara wa
juu sana barani Africa .
Wabunge
walifurika katika jengo hilo
lililokarabatiwa wakati rais na spika wakiongoza utaratibu wa sherehe za
ufunguzi.
Ukarabati
huo ulianza mwezi Aprili mwaka 2010 na ulikuwa umepangwa kuchukua mwaka mmoja
kumalizika lakini ulichelewa kwasababu ya utata ulioghubika zabuni yake,
mwandishi wetu anasema.
Mbunge
John Mbadi, katika kamati ya uwekezaji aliongoza upinzani juu ya zabuni ya
kwanza.
"hatukuweza
kuelewa ni kwa vipi wabunge wangekuwa wanakaa katika viti vinavyogharimu karibu
shilingi 400,000 za Kenya kama dola 5,000, ambazo kwa kiwango chochote cha
kawaida zingeweza kujenga nyumba kwa wananchi kadhaa," ameiambia BBC.
"ilikuwa
ni upuuzi," amesema.
Mwandishi
wetu anasema watu wengi wamelalamika kuwa gharama za sasa bado ni juu.
David
Langat, anayesimamia uzalishaji katika magereza nchini Kenya , amesema vifaa vyote vilivyotumika
vilitoka nchini Kenya lakini
gharama za viti zimekuwa kubwa sana .
Ameiambia
BBC kuwa viti hivyo vyenye uzito wa kilo 50 kila kimoja vina kinga dhidi ya
moto na vina dhamana ya miaka 30.
Kwa
sasa Kenya
ina jumla ya wabunge 220 lakini ukumbi huo umewekwa viti 350 idadi ambayo
watachaguliwa katika uchaguzi ujao mwezi Machi kwa mujibu wa katiba mpya.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment