Safari ilianzia kwenye Tawakal saa moja asubuhi. Tulipokea taarifa za msiba Mzee Shehe amefariki, ni Baba yangu mdogo maana amemuona mama yangu Mkubwa. Hivyo ni baba yangu sikuwa na budi lazima nirauke na siku hiyo ya alhamisi kuamkia Ijumaa tulilala Lugalo kambi ya Jeshi kwa dada Safina, mtoto mkubwa wa Marehem. Nilikuwa mimi na kamanda wangu Chuse, mtoto wa mama mkubwa Zainab Katani, baba mmpja na mama yangu Rehema Katani.
Mara baada ya kuvuka daraja la Wami tukaona msururu wa magari, tulipouliza tukaambiwa kuna ajali imetokea kijiji cha jirani, nimwendo wa dakika arubaini mpaka nusu saa kwa mtu anaetembea kijeshi, ila mtu legelege inaweza kumchukua saa nzima kufika eneo la tukio kwa mguu kutoka msururu wa magari ulipoanzia.
Huyo kijana mwenye fulana nyekundu anaitwa Abdul Zauya, ni mtoto wa baba mdogo nae alipanda Tawil, tukakutana kwenye msururu huo bila kutarajia tukaamua tutembee tukashuhudie ajali kama kuna msaada tutoe.
Tukiwa njiani tukashuhudia mzee akiishiwa nguvu mpaka akaamua kupunguza njaa kwa kununua kinywaji.
Hata Raia wa kigeni nae alitaka kushuhudia ila aliishia njiani. Alipokuwa anardi nilimuuliza kwa kimombo kuwa aliiona ajali hata hakujisumbua kunijibu. Sijui alichoka ama ujeri tu.
Safari inaendelea, tulitaka kukata tamaa lakini tukashauriana hakuna haja ya kurudi maana tulishtembe vya kutosha. Ingawa tulikuwa tumefunga lakini tukajikaza kisabuni huku tunatoka mapovu.
Hata wanakijiji wenyewe wakawa wanashangaa umati wa watu walishazoea kuona watu wengi kipindi cha kuomba kura.
Hatimae tukapishana na gari lililobeba maiti 14 waliokuwamo katika ajali, hakika mwili ulinisisimka kwa hofu
Mama Mantumu mahiza nae alikuwepo eneo la ajali kutimiza wajibu wake akiwa mkuu wa mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment