Safari bado inaendelea, njia nikakutana na Bus la Kampala Coach, nikawaonea huruma sana, maana hiyo ilikuwa ni saa sita mchana na Bus iliondoka Dar es Salaam saa 12 alfajiri. Ilitakiwa kufika wami saa tatu asubuhi mpaka saa saba ilikuwa hapo. Unadhani Kampala itafika saa ngapi? hakika niliwapa pole. Maana ilitakiwa kufika kampala kesho jumamosi saa saba mchana, sasa ipo nyuma kwa saa zaidi ya nne, maana yake saa saba mchana ongeza saa nne mbele itafika saa ngapi?
Nikakutana na wanafunzi wa KIU Kampala ambao walikuwa katika Kampala Coach wakirudi Chuoni baada ya likizo, huyu wa mwanzo kutoka kushoto namfahamu sana ila jina limenitoka, nilimuacha chuoni mwaka wa kwanza, tena ni mbunge wa chama cha watanzania hapo chuoni. wa pili simjui na wa tatu namfahamu sana ila jina pia limenitoka. Samahani sina kawaida ya kumuuliza mtu 'hebu nikumbushe jina lako' maana huyu wa kwanza aliponiona tu akaruka 'haaa kaka kido mambo?' Naam ananiita kaka maana wakati ninamaliza chuo nilikuwa Mwenyekiti wa Watanzania hapo chuoni na nilijiheshimu hivyo nikawa naheshimika....
Hatimae tukafika eneo la ajali, hakika ajali ilikuwa mbaya ilihusisha magari manne. Mawili yalitumbukia kwenye korongo (ditch), na mawili yakaziba njia, ndiyo maana magari yakakaa muda mrefu kuyasubiri.
hatimae baada ya kuwaondoa maiti na majeruhi eneo la tukio jitihada za kufungua njia zikaanza na kweli nijia ikafunguka ilipofika saa saba mchana. Safari ikaanza upya kwa kila msafiri...
Jembe nikapiga stand up reporting.. nikiripoti kutoka wilaya ya bagamoyo mimi ni..
Hki ni kikosi kazi ambacho kilikuwa kikiopoa waliokufa na majeruhi. Lakini pia walikuwa na kazi nyingine ya kuwaonyesha madereva wenye haraka kupita njia za porini. Maana kukaa sehemu zaidi ya saa sita si kazi ndogo. nitakuonyesha magari yaliyofanikiwa kupita kutokana na juhudi za kikosi kazi hiki. Kufa kufaana...
No comments:
Post a Comment