Kamanda wa kikosi cha kuzuia dawa za Kulevya nchini Godfrey Nzowa, akionyesha pasi ya kusafiria ya Muindonesia huyo aliekamatwa jana.
Huyu ndie Mychel Takahindangeng, ambae amekamatwa jana katika uwanja wa ndege wa kimataifa JK Nyerere akisafirisha dawa za kulevya kilo nne zenye gharama za milioni 200.
Hizi ndizo dawa za kulevya kilo 4 ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika sanduku tayari kwa kusafirishwa kuelekea Vietnam kwa ndehge ya Oman Airlines jana saa tisa alasiri. Katika pasi yake ya kusafiria yenye namba A2915930 iliyotolewa tarehe 07/06/2012 inaonyesha nchi alizotembelea hivi karibuni ni China, India, Timori Mashariki na Tanzania.
No comments:
Post a Comment