Wananchi wakiwa katika sura za mshangao baada ya kusubiri kwa muda mrefu bila matumaini.
Nenda ukasajiliwe upate kitambulisho chako kabla ya wikimbili kuisha.
Mzee Mneka huyu, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa, Alimaua B.
Malalamiko yameanza katika
mchakato wa kupata vitambulisho vya Taifa. Leo nikiwa katika kituo cha
kijitonyama alimaua B, nilikutana na changamoto hizo za malalamiko ya utaratibu
mbaya wa kupata vitambulisho hivyo.
Sikutaka kufanya mahojiano na
wadau hao maana sikutaka wajue mimi ni mwanahabari, lakini kwa ujumla
malalamiko makubwa ni makarani kuwa taratibu katika kuchukua maelezo na wengi
wao wakilalamika elimu ndogo ya makarani hao.
Kadhalika wafanyakazi wa
serikali na binafsi walitoa ushauri ni kwanini wafanyakazi hao wa NIDA wasitoe
fomu hizo katika ofisi ili kutoa urahisi na kuokoa muda. Maana kwa utaratibu wa
sasa siku ya kwanza unajaza fomu halafu unarudi tena kuambiwa kuwa maelezo yako
yamekubaliwa kwa ajili ya kupewa kitambulisho maana mpaka kikatengenezwe.
Hivyo kama ni mfanyakazi
ambae unatoka asubuhi na kurudi jioni itakuwa vigumu kusubiri foleni ambayo kwa
hakika ni ndefu. Nadhani ipo haja NIDA wakasikiliza matatizo ya wadau kuliko
kujitia uziwi wasiokuwa nao.
HAFIDH KIDO
0713 593894/ 0752 593894
DAR ES SALAAM , TANZANIA
hafidhkido@yahoo.com
KUTOKANA NA UNYETI WA KAZI HII WANANCHI TANATAKIWA KUWA NA SUBRA....!!!!!!
ReplyDeleteVYENGINEVYO VITAMBULISHO VINAWEZA KUANGUKIA KWA WASIO WALENGWA....!