Jembe langu Said makala wa Chennel ten akiwa na vifaa vya kazi eneo la tukio makao makuu ya chadema leo. Nilikuwa nae New Habari mwaka 2008 huyu.
Chama cha demokrasia na
maendeleo wamekanusha kuhusika na vurugu zilizotokea katika jimbo la kada wa
CCM Mwigulu Nchemba na kusababisha kifo cha mtu mmoja kada wa UVCCM katika
kijiji cha ndago.
Akizungumza na wanahabari
katika makao makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam, leo mchana afisa wa
sera na utafiti Waitara Mwita, anasema walitoa taarifa mapema kuhusiana na
kuzuka kwa vurugu hizo lakini mkuu wa kituo cha Ndago alipuuzia.
“Sisi wanatuambia ndiwo
tulioanzisha vurugu lakini si kweli, wakati tunaanza kupigwa mawe OCS wa Ndago
alikuwepo na tukaamua kumpigia mkuu wa polisi mkoa wa Singida amabae alileta
ulinzi lakini polisi hawakufanya chochote zaidi ya kuangalia tu. Sisi
(chadema), tulitaarifiwa juu ya watu wawili ambao walisafiri mpaka Dodoma kuchukua pesa za
kuendeshea vurugu kutoka kwa mbunge wa Iramba Mashariki Mwigulu Nchemba, na
tukatoa taarifa polisi lakini hakuna kilichofanywa,” alisema.
Hata hivyo inaelezwa kuwa
mbali ya watu wa vijiji vya karibu kuja kuhudhuria mkutano huo kwa minajili ya
kufanya vurugu lakini inadaiwa kuna vijana tisa ambao walitoka mjini Dar es
Salaam kwa lengo hilo
tu la kuvuruga mkutano wa chama hicho.
Kwa maelezo ya Waitara ambae
ni miongoni mwa watuhumiwa wa mauaji katika vurugu hizo hawaafikiani na jeshi
la polisi kutoa taarifa za uongo kwani wakati alipokuwa ameshikiliwa na jeshi
hilo alishuhudia wafuasi wa chama cha CCM ambao walikamatwa kuhusiana na kesi
hiyohiyo kuachiwa huru bila kufuata utaratibu na kumuacha mmoja tu, hata wale
tisa waliotoka Dar es Salaam, waliwekewa dhamana katika mazingira ya rushwa.
“sisi hatukubaliani nakesi
hiyo na tunataka kuundwa kwa tume huru ambayo itachunguza suala hilo ,maana sisi tunayo
filamu ya tukio zima lakini hatuwezi kuikabidhi kwa jeshi la polisi maana
hatuwaamini,” alieleza Waitara.
HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM , TANZANIA
25/07/2012
No comments:
Post a Comment