Kama kawaida yangu nawakaribisha tena katika ukurasa huu kuweza kuwaletea futari tutakayopika wakati wa jioni kwa ajili ya kupata afya na kuondoa njaa.
Leo tutapika chapati, mihogo, sambusa, bhajia (za kunde ama dengu), choroko za maua (kwa wanozijua), na ndizi mbivu za nazi (mkono wa tembo). Tutapika mchuzi wa kukaanga wa viazi kwa ajili ya chapati (usitie nyama). Kitoweo kitakuwa samaki.
kama kawaida usisahau matunda, na maji ya kutosha maana kama unavyotambua mwili wa binaadam unahitaji maji mengi ili kulainisha chakula. Kwasababu tukifunga tunakaa zaidi ya saa kumi na mbili bila ya kunywa maji ni vema tuutumie muda wa futari kunywa maji ya kutosha.
HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
26/07/2012
No comments:
Post a Comment