Fatou Bensouda, mwendesha mkuu wa mashtaka katika mahakama ya
kimataifa ya jinai, ICC. Bensouda mwenye umri wa miaka 51, aliteuliwa katika
wadhifa huo mwezi Juni mwaka huu na kuchukua nafasi ya Luis Moreno-Ocampo
kutoka Argentina.
Kabla ya hapo Bensouda alikuwa naibu mwendesha mkuu wa mashtaka tangu mwaka
2004.
Ellen Johnson-Sirleaf, rais wa Liberia
ana umri wa miaka, 72 na alitajwa kama mshindi
wa tatu wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2011. Tuzo hiyo imetolewa miaka sita
baada ya yeye kuchaguliwa rais wa Liberia na kumfanya kuwa rais wa
kwanza mwanamke barani Afrika.
Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenyekiti wa tume ya muungano wa
Afrika. Alichaguliwa tarehe kumi na tano mwezi Julai baada ya kinyang'anyiro
kikali kati yake na mwenyekiti wa zamani Jean Ping. Bi Dlamini-Zuma, mwenye
umri wa miaka 63, ni mwanamke wa kwanza kuwahi kushikilia wadhifa huo.
Ngozi Okonjo-Iweala, waziri wa fedha wa Nigeria. Bi Okonjo-Iweala, mwenye
umri wa miaka 58, ameshikilia nyandhifa mbalimbali za kimataifa, katika sekta
ya fedha .Aliheshimika sana
wakati akiwa mkurugenzi mkuu katika benki ya dunia kwa miaka mitatu, kabla ya
kushindana katika kinyang'anyiro kuwa rais wa benki hiyo.
Joyce Banda, rais wa Malawi. Bi Banda mwenye umri wa
miaka 62, amefannya jambo la kihistoria kwa kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini
humo. Pia yeye ni mwanamke wa pili kuongoza nchi ya ya kiafrika. Anaheshimika
kakam mwanaharakati wa haki za wanawake.
No comments:
Post a Comment