Jamaa mmoja mida hii
chupuchupu agombewe na wanachama wa Yanga, baada ya kufika makao makuu ya
klabu, Jangwani akiwa na barua ya wakili inayoshauri uchaguzi wa klabu hiyo uliopangwa
kufanyika Jumapili wiki hii uahirishwe.
Kilichomponza ni
kwamba, alipofika mlango wa kuingia klabuni, akasema anataka kumuona Katibu
Mkuu, ana barua ya Mahakama ya kuzuia uchaguzi.
Watu kusikia hivyo
wakamvaa, kwanza wakampora begi lake
wakachukua barua
wakaisoma. Wakagundua ni ya wakili tu na haina nguvu, ndipo wakamrudishia barua
yake na kumfukuza, tena wakimuonya asionekane kabisa katika viunga hivyo. Soma
barua yenyewe….
Chanzo:
www.bongostaz.blogspot.com



No comments:
Post a Comment