Friday, July 13, 2012

Kamera yetu mtaani leo.

 Wakati nikielekea ofisini leo asubuhi nikakutana na huyu mama akibandika tangazo la kuuza ice cream, mtaani tunaita 'ashkrimu' ama barafu.Naam biashara matangazo.

                                     Huyu mtoto anapuliza moto sasa sijui anataka kupika nini.

 Huyu mtoto alinifurahisha sana, aliniona nimebeba kamera akaniambia 'kaka nipige pichaa' nami sikumfanyia hiyana.

 Hawa jamaa wanagombania mihogo niliwanasa na kamera yangu asubuhi hii. Mtaani kwetu mihogo ndiyo mwokozi wa wanywa chai.

Jamaa akipanga viatu na vifaa vingine, naam ukijituma utapata chochote kitu.

No comments:

Post a Comment