Na Hafidh Kido
Leo nimechelewa kuwapatia
habari na jana sikuonekana kabisa, si lengo langu kufanya hivyo lakini hali ya
maisha inanifanya naelemewa na jukumu hili la kuwapasha kinachojiri
ulimwenguni.
Siku ya jana yaani jumapili
ilikuwa siku fupi sana kwangu, sikupata muda wa
kutembelea hata ukurasa wangu wa facebook, zaidi ya neno la leo kilichofuata ni
kuandika kuhusu kuonewa na Spain
katika fainali. Hakika ule ulikuwa ni uonevu 4 mtungi?
Siku ya leo nilifika ofisini
mapema saa tatu nikiwa na picha zangu za kutosha kuweza kuwapasha wadau wangu,
nikapata muda wa kupata kikombe cha chai tupu ya mkandaa huku nikipitia
magazeti na baadhi ya blogu ninazoziamini zitanipatia habari za kutosha.
Nikijiandaa kuingia kazini kuwapasha
nilichopata mara huduma ya mtandao (internet) ikawa chini, mara ikakata
kabisaaa. Kuwauliza watu wa DTP wakanambia mtandao umeisha pesa. Lahaulaaaa….
Haya ndiyo matatizo ya
kupenda mserereko(bure), yaani mserereko mpaka katika kuendesha blogu? Kweli
maisha magumu.
Ndugu zangu, ninayo modem ya
kuendeshea blogu hii lakini ni gharama sana ,
ofisini natumia mtandao wa bure, na ndiyo sababu leo nimechelewa kuonekana,
poleni kwa usumbufu. Niombeeni jembe lenu nionekane na wadhamini wanipatie
vijisenti vya kuendeshea blogu yenu ya jamii.
HAFIDH A. KIDO
0752 593894
DAR ES SALAAM , TANZANIA
No comments:
Post a Comment