Ndugu Wananchi,
Usafirishaji Haramu wa
Binadamu Nchini
Ndugu Wananchi;
Bila ya shaka mtakuwa
mmezisikia taarifa za tukio la kushtusha na kuhuzunisha la kukutwa maiti 43 za
watu wasiojulikana, zilizotupwa katika kichaka kilichopo kijiji cha Chitego,
Wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma tarehe 26 Juni, 2012. Pamoja na maiti hao,
walipatikana watu 84 wakiwa hai lakini wote wakiwa wamedhoofu na baadhi yao wakiwa mahututi.
Hatua za haraka zilichukuliwa kuwasafirisha watu hao hadiDodoma
ambapo wale waliokuwa mahututi walifikishwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu na wengine walihifadhiwa katika Kituo
cha Kati cha Polisi, Dodoma .
Maiti 22 zilipelekwa Dodoma
na 21 zilipelekwa Morogoro kuhifadhiwa.
Hatua za haraka zilichukuliwa kuwasafirisha watu hao hadi
Taarifa zilizopatikana
kutoka kwa wale walionusurika zimebainisha kuwa watu hao ni raia wa Ethiopia ambao walikuwa safarini kwenda Malawi
na baadaye Afrika ya Kusini ambako wangetengenezewa utaratibu wa kwenda kuishi
Marekani na Ulaya. Kwa mujibu wa maelezo yao ,
safari yao
ilianza miezi mitano iliyopita. Mwezi mmoja waliutumia Ethiopia na miezi minne waliitumia Kenya kabla ya kuletwa Arusha ambako walipakiwa
kwenye lori na kuanza safari ya kuelekea Malawi lakini ikaishia Chitego.
Lori walilopanda lilikuwa limezibwa kabisa na hivyo kusababisha vifo kwa kukosa hewa.Tukio la Chitego,Dodoma
la wahamiaji haramu kukamatwa na wengine kukutwa wamekufa si la kwanza kutokea
hapa nchini. Kwa jumla, katika kipindi cha takriban miaka 10 sasa kumekuwepo na
tatizo kubwa la wahamiaji haramu kuingia nchini. Kwa mfano, kati ya mwaka 2005
na hivi sasa jumla ya wahamiaji haramu 19,683 wamekamatwa.
Karibu wote wameshaondoshwa nchini na hivi sasa wapo karibu watu 1,500 tu magerezani wanaotumikia adhabu na kusubiri kurejeshwa makwao. Wengi wa watu hao wanatokaEthiopia na Somalia
na baadhi kutoka Pakistan na
Bangladesh .
Lori walilopanda lilikuwa limezibwa kabisa na hivyo kusababisha vifo kwa kukosa hewa.Tukio la Chitego,
Karibu wote wameshaondoshwa nchini na hivi sasa wapo karibu watu 1,500 tu magerezani wanaotumikia adhabu na kusubiri kurejeshwa makwao. Wengi wa watu hao wanatoka
Wahamiaji haramu
wamekuwa wanaingia nchini kwa kupitia njia zisizo rasmi. Wapo wanaotumia nchi
kavu hasa kupitia mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga. Na, wapo
wanaopitia baharini kwa kutumia fukwe za Pemba ,
Unguja na za mikoa ya ukanda wa Pwani ya Tanzania Bara yaani Tanga, Pwani,
Lindi na Mtwara.
Ndugu Wananchi;
Kwa mujibu wa kauli zao,
watu hao wamekuwa wanaeleza kuwa hawaji nchini kuhamia bali wao ni wapita njia
tu. Wanaelekea Afrika ya Kusini ambako wameahidiwa kuwa watatengenezewa mipango
ya kuhamia Marekani na Ulaya. Watu hao pia wamethibitisha kuwepo kwa watu
maalum wanaojihusisha na usafiri wao tangu nchi watokako na zote wanazopitia
mpaka kule waendako. Aidha, wamesema kuwa wao wanawalipa watu hao ili
wawasafirishe na hakika si kiwango kidogo. Kwa jumla ni kwamba hili si suala la
uhamiaji haramu bali ni la biashara haramu ya kusafirisha binadamu.
Ndugu Wananchi;
Kufuatia vyombo vyetu
vya usalama kuwa makini na watu wengi kukamatwa ndipo wasafirishaji walipobuni
njia za kuwasafirisha kama mizigo. Makontena,
malori yaliyofunikwa nyuma na matenki ya mafuta na ya maji yamekuwa yanatumika
kwa ajili hiyo. Usafiri wa aina hiyo ndiyo uliosababisha vifo vilivyotokea
Dodoma tarehe 26 Juni, 2012 na vya watu 21 vilivyotokea mwezi Desemba, 2011
Mkoani Morogoro, na vile vya watu 12 vilivyotokea katika matukio mawili ya Mkoa
wa Mbeya, mwezi Mei, 2012.
Ndugu Wananchi;
Tarehe 27 Juni, 2012
nilikutana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuzungumzia tukio la
Chitego na suala zima la biashara hii haramu na hasa mbinu mpya inayotumiwa na
wasafarishaji. Nilitoa pongezi kwa vyombo vya dola kwa kazi nzuri waifanyayo
kudhibiti shughuli za biashara hii haramu hapa nchini. Tulielewana kuwa
waendelee kuimarisha udhibiti huo kwa lengo la kukomesha kabisa biashara hii.
Niliagiza pia kwamba
kikundi kazi nilichokiunda mwaka 2006 kushughulikia ujambazi sasa kielekeze sehemu
ya nguvu zake kukabili tatizo hili. Aidha, kwa pamoja tulikubaliana kuwa nchi
yetu ishirikiane na wenzetu wa Ethiopia ,
Kenya , Malawi , Msumbiji na Afrika ya
Kusini kutambua mawakala na kuwabana kwa mujibu wa sheria.
Tayari nimeshaanza kufanya mawasiliano na baadhi ya Wakuu wa Nchi hizo kuhusu ushirikiano huo. Nashukuru wote wameafiki nchi zetu zishirikiane kwa pamoja kuvunja mtandao huu mchafu na kutokomeza biashara hii haramu na inayodhalilisha utu wa mwanadamu.
Tayari nimeshaanza kufanya mawasiliano na baadhi ya Wakuu wa Nchi hizo kuhusu ushirikiano huo. Nashukuru wote wameafiki nchi zetu zishirikiane kwa pamoja kuvunja mtandao huu mchafu na kutokomeza biashara hii haramu na inayodhalilisha utu wa mwanadamu.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuchukua nafasi
hii kuwashukuru wenzetu, wakazi wa vijiji vya Chitego na Mkoka kwa kazi nzuri
walioifanya. Kwa kweli, wenzetu wameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kutoa
taarifa mapema juu ya jambo lenyewe, lakini pia wameonesha utu kwa kuwajali
wageni waliokumbwa na janga hili. Naushukuru pia uongozi wa Mkoa wa Dodoma na
Morogoro ikiwa ni pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kulishughulikia
tatizo hilo kwa umakini mkubwa. Nimefurahishwa sana na ushirikiano ulioonyeshwa na vyombo na
taasisi mbalimbali za Serikali katika kushughulikia suala hili.
Mgomo wa Madaktari
Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ni kuhusu
mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini hivi sasa. Nilipozungumza na Wazee wa Dar
es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 12 Machi, 2012, kuhusu mgomo
wa Madaktari uliokuwa unaendelea wakati ule pamoja na kuelezea chimbuko la
mgomo na hatua iliyokuwa imefikiwa, nilielezea mazungumzo yangu na viongozi wa
Chama cha Madakari wakiwemo pia viongozi wa Jumuiya ya Madaktari. Nilitoa
taarifa kuwa tumeelewana kuwa watasitisha mgomo na watarudi kwenye meza ya
majadiliano na Serikali. Siku ile pia nilielezea matumaini yangu kuwa mgomo ule
utakuwa wa mwisho katika nchi yetu. Bahati mbaya matumaini yangu hayo hayakuwa
na hivi sasa tunashuhudia tena wagonjwa wakiteseka, kuhangaika na wengine kufa
kwa sababu ya kukosa huduma wanazostahili kwa vile madaktari wao wamegoma tena.
Ndugu Wananchi;
Ndugu Wananchi;
Kati ya tarehe 10
Aprili, 2012 na tarehe 30 Mei, 2012, vilifanyika vikao sita vya majadiliano
kati ya Serikali na Chama cha Madaktari. Katika mazungumzo hayo hoja au madai
12 ya madaktari yalizungumzwa. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
1. Posho ya kuitwa
kazini (on call allowance) iwe asilimia 10 ya mshahara.
2. Posho ya kufanya kazi
katika mazingira hatarishi (Risk allowance) iwe asilimia 30 ya mshahara.
3. Madaktari wapatiwe
nyumba grade A au posho ya makazi ambayo iwe asilimia 30 ya mshahara.
4. Posho ya kufanya kazi
katika mazingira magumu iwe asilimia 40 ya mshahara.
5. Madaktari walipwe
posho ya usafiri ya asilimia 10 ya mshahara au wakopeshwe magari.
6. Madaktari wanaoanza
kazi walipwe mshahara wa shilingi 3,500,00/= kwa mwezi.
7. Madaktari wapatiwe
Green Card za Bima ya afya.
8. Hatua za kinidhamu
zichukuliwe dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
9. Viongozi wa Kisiasa
kulazimisha kupewa rufaa nje.
10. Madaktari
waliofukuzwa warudishwe kazini.
11. Huduma za afya
ziboreshwe nchini.
12. Posho ya uchunguzi
wa maiti iongezwe.
Ndugu Wananchi;
Katika mambo hayo 12
pande zote mbili zilifikia muafaka na kukubaliana wa pamoja kwa mambo saba. La
kwanza, ni kuhusu usafiri wa kwenda na kurudi kazini. Serikali ilieleza kuwa
upo utaratibu kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi wa Serikali Na. 3 wa mwaka 2011
wa kuwakopesha wafanyakazi wa Serikali fedha za kununulia magari au pikipiki, samani
na matengenezo ya magari. Ilikubaliwa kuwa madaktari waitumie fursa hiyo.
Jambo la pili, ni kuhusu
madaktari kupatiwa Green Card za Bima ya Afya. Jambo hili lilikubaliwa na
Serikali na Wizara ya Afya imekwishachukua hatua za utekelezaji wake.
Jambo la tatu, ni kuhusu
hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya. Kwa
pamoja walikubaliana kuwa suala hilo liko nje ya
mamlaka ya Kamati yao
ya pamoja, waziachie mamlaka husika za uteuzi.
Uongozi wa juu wa Wizara umebadilishwa na sasa kuna uongozi mpya. Lakini, jambo la kustaajanisha hata Waziri mpya wa Afya alipowataka waonane kuzungumzia hoja walikataa kumuona.Kwanza walisema hawaoni
sababu kwa vile wameyazungumza na Kamati yake kwa miezi mitatu bila ya
mafanikio
Uongozi wa juu wa Wizara umebadilishwa na sasa kuna uongozi mpya. Lakini, jambo la kustaajanisha hata Waziri mpya wa Afya alipowataka waonane kuzungumzia hoja walikataa kumuona.
Jambo la nne walilokubaliana
ni kuhusu viongozi kulazimisha kupewa rufaa ya kutibiwa nje. Walikubaliana
mambo mawili. Kwanza , kwamba maelekezo ya
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kuwa madaktari wazingatie maadili ya kazi zao
na kukataa kutoa rufaa kwa mtu asiyestahili awe kiongozi au asiwe kiongozi.
Pili, walikubaliana kuwa hospitali zilizopo ziboreshwe ili viongozi watibiwe
hapa nchini. Ukweli ni kwamba kufanya hivyo ndiyo sera ya Serikali. Nililieleza
hili mwezi Desemba 30, 2005 katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge baada ya
kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza nchi yetu.
Tumeiongeza sana bajeti ya sekta ya
afya kutoka shilingi bilioni 300 2005/2006 hadi shilingi trilioni 1.2 mwaka
2011/12 na imekuwa ya tatu baada ya miundombinu na elimu. Tumeziimarisha
hospitali za Mikoa kwa vifaa tiba na wataalamu wa afya. Kazi inaendelea katika
hospitali za Wilaya. Tumewekeza katika Hospitali ya Muhimbili.
Hospitali hiyo ilivyo leo sivyo ilivyokuwa miaka sita nyuma. Na kazi inaendelea hasa katika maeneo ambayo tunapeleka wagonjwa nje. Matunda yake yanaanza kuonekana kwa upande wa figo, moyo, kinywa na mipango inaendelea kwa upande wa ubongo na mishipa ya fahamu. Tunaendelea kuimarisha mafunzo ya madaktari na madaktari bingwa, yote kwa nia hiyo hiyo. Hivi sasa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba,Muhimbili kinachukua wanafunzi wengi zaidi ya ilivyokuwa siku za nyuma na makazi mapya ya chuo yanaendelea kuandaliwa ili kuchukua wanafunzi wengi zaid. Mwaka 2005 tulikuwa na madaktari bingwa 46 mwaka huu tunao 520.
Hospitali hiyo ilivyo leo sivyo ilivyokuwa miaka sita nyuma. Na kazi inaendelea hasa katika maeneo ambayo tunapeleka wagonjwa nje. Matunda yake yanaanza kuonekana kwa upande wa figo, moyo, kinywa na mipango inaendelea kwa upande wa ubongo na mishipa ya fahamu. Tunaendelea kuimarisha mafunzo ya madaktari na madaktari bingwa, yote kwa nia hiyo hiyo. Hivi sasa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba,Muhimbili kinachukua wanafunzi wengi zaidi ya ilivyokuwa siku za nyuma na makazi mapya ya chuo yanaendelea kuandaliwa ili kuchukua wanafunzi wengi zaid. Mwaka 2005 tulikuwa na madaktari bingwa 46 mwaka huu tunao 520.
Ndugu Wananchi;
Jambo la tano ambalo
pande zote mbili zilikubaliana ni kuhusu madaktari waliofukuzwa. Hawa ni wale
Interns waliokuwa wamerudishwa Wizarani kutoka Muhimbili na kupangiwa hospitali
za Temeke, Ilala, Mwananyamala na Lugalo. Hili ni jambo ambalo lilikuwa
limemalizika kitambo na wote walikuwa wamerudi Muhimbili.
Jambo la sita ni kuhusu
mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na madaktari kuhusu kuboresha huduma ya
afya. Mapendekezo hayo yalihusu kutathmini sera na mpango wa afya ya msingi,
bajeti ya afya kuwa asilimia 15 ya bajeti ya Serikali, kuwepo na utaratibu
mzuri wa kuajiri madaktari na kuboresha viwango vya ubora wa madaktari na
kadhalika. Serikali imeyaafiki mapendekezo hayo na yatafanyiwa kazi.
Jambo la saba, ambalo
pande zote walilokubaliana ni kuhusu kuongeza posho ya uchunguzi wa maiti. Hili
ni jambo jipya halikuwepo mwazoni. Hata hivyo, Serikali imelikubali na posho
hiyo imeongezwa kutoka shilingi 10,000/= hadi kufikia shilingi 100,000/= kwa
daktari na shilingi 50,000/= kwa wasaidizi wake.
Ndugu Wananchi;
Kuna masuala matatu
ambayo yamekuwa na muafaka kwa kiasi fulani na kutoafikiana kwa baadhi ya
mambo. La kwanza ni suala la kufanya kazi katika mazingira hatarishi. Serikali
imekubali hoja ya kuchukua hatua ya kuwalinda madaktari wanaofanya kazi katika
mazingira hatarishi. Serikali iliwaeleza kuwa watumishi wa kada zote za afya
watapatiwa chanjo dhidi ya maambukizi ya Hepatitis B na fedha zimetengwa katika
bajeti ya 2012/13.
Aidha, Serikali imeeleza
dhamira ya kurudisha posho ya mazingira hatarishi kwa watumishi wa umma
wanaostahili. Utekelezaji wake utafanyika baada ya uchambuzi wa kina wa
kubainisha mazingira hatarishi ni yepi, viwango stahiki viwe vipi na nani hasa
wahusike. Madaktari wamekataa hili la kufanya uchambuzi, wanataka kiwango kiwe kama wanavyotaka wao, yaani asilimia 30 ya mshahara na
kianze mara moja.
Jambo la pili ambalo
wamekubaliana nusu nusu ni kuhusu nyumba za kuishi. Serikali imekiri wajibu
wake wa kuwapatia madakari nyumba za kuishi. Aidha, imeeleza mpango ulioanza wa
kujenga nyumba 700 za madaktari kote nchini na kwamba hivi sasa ujenzi wa
nyumba 90 unaendelea, 50 katika mkoa wa Mtwara na 40 katika mkoa wa Rukwa.
Kwa maeneo ambayo
madaktari wanalipwa posho ya pango Serikali imesema waajiri wataendelea kufanya
hivyo kwa mujibu wa taratibu zilizopo kwa watumishi wa umma wenye stahili ya
kupewa nyumba. Jambo hilo limekataliwa na
Madakari na kutaka lazima walipwe asilimia 30 ya mshahara kama
posho ya nyumba. Serikali kwa upande wake imeona vigumu kufanya hivyo na
kuwasihi wakubali wanayotendewa wafanyakazi wengine wote wa umma.
Jambo lingine ambalo lilikuwa na makubaliano ya nusu nusu ni kuhusu posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu. Pande zote mbili ziliafikiana kuwa yapo baadhi ya maeneo nchini yanayo mazingira magumu kwa watumishi wa umma hivyo hatua zichukuliwe kuwasaidia watumishi hao. Serikali imekubali wajibu wa kuweka utaratibu wa kuboresha maisha ya watumishi katika maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, Serikali itatoa mwongozo kwa mamlaka za ajira kuhusu namna ya kuwasaidia watumishi hao kupunguza makali ya maisha katika kila eneo badala ya kutegemea posho peke yake.
Jambo lingine ambalo lilikuwa na makubaliano ya nusu nusu ni kuhusu posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu. Pande zote mbili ziliafikiana kuwa yapo baadhi ya maeneo nchini yanayo mazingira magumu kwa watumishi wa umma hivyo hatua zichukuliwe kuwasaidia watumishi hao. Serikali imekubali wajibu wa kuweka utaratibu wa kuboresha maisha ya watumishi katika maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, Serikali itatoa mwongozo kwa mamlaka za ajira kuhusu namna ya kuwasaidia watumishi hao kupunguza makali ya maisha katika kila eneo badala ya kutegemea posho peke yake.
Kuhusu posho, Serikali
imeeleza kuafiki kuwepo posho ya aina hiyo ila itatekelezwa baada ya kufanya
uchambuzi wa kuainisha mazingira husika, kutambua watumishi waliopo na gharama
zake.
Madaktari hawajakubali
kusubiri zoezi la uchambuzi lifanyike, wanataka Serikali ilipe posho hiyo sasa.
Tofauti hapa si posho hiyo kuwepo, bali ni rai ya Serikali ya kubaini maeneo
yenyewe na kupanga aina ya hatua na viwango vya posho kulingana na mazingira
halisi ya maeneo. Madaktari hawaoni haja ya kufanya hayo.
Ndugu Wananchi;
Mambo mawili hayakuwa na
muafaka kabisa kati ya pande zetu mbili. Jambo la kwanza ni posho ya kuitwa
kazini (on call allowance). Kwanza sina budi
kueleza kuwa Serikali imekubali kuongeza posho hiyo. Tangu Februari, 2012 posho
iliongezwa kutoka shilingi 10,000/= hadi shilingi 25,000/= kwa daktari bingwa
(Specialist), shilingi 20,000/= kwa dakari mwenye usajili wa kudumu
(Registrars) na shilingi 15,000/= kwa madaktari waliohitimu ambao wapo katika
kipindi cha mafunzo kazini (Interns). Viwango hivyo vya posho vinatumika hivi
sasa.
Madaktari kwa upande wao
hawakukubali uamuzi huo wa Serikali na kusisitiza walipwe asilimia 10 ya
mshahara. Ugumu wa kukubali pendekezo la madakari ni kuwa sharti la malipo haya
ni mtu kuitwa kazini.
Ukitaka ilipwe kiwango cha mshahara ina maana kuwa hatakama
daktari hakupangwa kuitwa au alipangwa na hakutokea aendelee kulipwa. Hili
haliwezi kuwa sahihi kufanya. Linaweza kuwafanya baadhi ya madaktari kutokutimiza
wajibu wao kwa vile wana hakika mwisho wa mwezi malipo yako pale pale.
Ukitaka ilipwe kiwango cha mshahara ina maana kuwa hata
Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ambalo
muafaka haukufikiwa baina ya Serikali na madaktari ni kuhusu mshahara wa
kuanzia kazi wa daktari. Madaktari wanataka uwe shilingi 3,500,000/= wakati
Serikali inasema kiasi hicho hatukiwezi. Serikali imeeleza utayari wake wa
kuongeza mshahara kwa kati ya asilimia 15 mpaka 20 kama
ambavyo itafanya kwa watumishi wote wa umma katika mwaka huu wa fedha. Kwa
kiwango cha sasa cha mshahara wao, daktari ataanzia kati ya shilingi
1,100,000/= na 1,200,000/= kutegemea kiwango kipi hatimaye kitaamuliwa.
Madaktari wamekataa katakata na wameng’ang’ania shilingi 3,500,000/=.
Ndugu Wananchi;
Huo ndiyo mlolongo wa
mambo yaliyozungumzwa na pande zote mbili na matokeo ya mazungumzo yenyewe.
Katika kikao cha sita kilichofanyika tarehe 30 Mei, 2012, upande wa Chama cha
Madaktari ulisema kuwa kwa vile hoja ya nyongeza ya mshahara haina mabadiliko
hawakuona haja ya kuendelea na majadiliano mpaka watakapowasiliana na wenzao.
Waliahidi kutoa taarifa ndani ya wiki mbili. Tarehe 12 Juni, 2012, Rais wa MAT
aliandika barua kwa Katibu Mkuu Utumishi ambaye ndiye kiongozi wa majadiliano
kwa upande wa Serikali, kuwa Madaktari wameikataa taarifa na ufafanuzi
waliopewa kutoka Serikalini kwa ujumla wake.
Ndugu Wananchi;
Baada ya majibu yale ya
madaktari, tarehe 19 Juni, 2012, Serikali na Madaktari walikwenda kwa
Msuluhishi (CMA) kutoa taarifa kuwa mgogoro umekosa usuluhishi kama sheria inavyotaka. Kwa pamoja pande zote mbili
zilikubaliana suala hilo
lifikishwe Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi. Wakati pande zote zinasuburi mgogoro
huu kufikishwa ngazi hiyo ya juu, upande wa Madaktari ukatangaza kuwepo kwa
mgomo kuanzia saa sita ya usiku tarehe 23 Juni, 2012. Hatua hiyo haikustahili
kwani suala lenyewe halijafika mwisho wa kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria za
Mahusiano ya Kazi nchini.
Ndugu Wananchi;
Tarehe 22 Juni, 2012,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali akaenda Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kulifikisha
suala la tishio la mgomo na kuomba zuio la muda kufanywa. Mahakama Kuu
ilikubali ombi hilo
na kuagiza kuwa mgomo usitishwe. Juhudi za kumtafuta Rais wa MAT, Dkt. Namala
Mkopi na viongozi wengine wa MAT hazikufanikiwa, Ofisi ya MAT ilikuwa imefungwa
na simu zote za viongozi wa MAT zilikuwa zimezimwa. Hatimaye tarehe 25 Juni,
2012, alipatikana na kupewa amri hiyo ya Mahakama. Tarehe 26 Juni, 2012, Dkt.
Mkopi alifika Mahakamani ambapo alikana kuwa yeye hahusiki na kuitisha huo
mgomo lakini hakumtaja aliyehusika. Pamoja na rai hiyo, Jaji alimuamuru Rais wa
MAT akawatangazie wanachama wake kusitisha mgomo. Dkt. Namala Mkopi hajafanya
hivyo hadi leo na mgomo umekuwa unaendelea kinyume cha Sheria.
Ndugu Wananchi;
Wagonjwa wanateseka na
wengine kupoteza maisha kwa mgomo huu usiokuwa halali kisheria ambao pia
haustahili kuwepo hata kwa mujibu wa maadili ya udaktari. Viongozi wa MAT na
wenzao wanawaingiza Madaktari katika mgogoro na Mahakama na waajiri wao
isivyostahili. Ni vyema viongozi wa Madaktari na madaktari wakatambua kuwa
wanashiriki katika mgomo usiokuwa halali ambao pia kiongozi wao mkuu amekana
Mahakamani kuwa hahusiki nao. Madaktari lazima watambue pia kwamba ajira zao
wanaziweka hatarini. Mfanyakazi ana kinga ya kutofukuzwa kazi na mwajiri kwa
kushiriki mgomo unaokubalika kisheria. Huu siyo. Watapoteza ajira, hawana pa
kukimbilia, hawana cha kiwalinda. Kwa madaktari interns, wanahatarisha maisha yao kwani hawatapata
cheti cha kudumu wakishiriki mgomo usiokuwa halali. Lazima watafakari sana kwa hayo
wafanyayo.
Ndugu Wananchi;
Napenda kurudia maneno
niliyoyasema tarehe 12 Machi, 2012, kuwa kuboresha mishahara na maslahi ya
wafanyakazi ni Sera ya Serikali yetu kwa maelekezo ya Ilani ya Chama Tawala
(CCM). Tumeitekeleza kwa vitendo sera hiyo, hata hivyo ni ukweli ulio wazi kuwa
nia yangu njema tu pekee haitoshi, lazima uwezo wa kufanya hivyo uwepo. Kwa
kulingana na uwezo uliopo, tumeendelea kuboresha mishahara na maslahi ya
wafanyakazi hatua kwa hatua tangu tuingie madarakani. Tumefanya hivyo kwa jumla
kwa wafanyakazi wote na kwa kada mbalimbali za watumishi wa umma.
Miongoni mwa wafanyakazi
wa umma walionufaika na hatua hizo za Serikali ni madaktari na watumishi wa
kada nyingine za huduma ya afya. Tena nadiriki kusema madaktari tumewapa
upendeleo mkubwa kuliko watumishi wengine wa umma. Upendeleo upo kwenye mafunzo
ambapo wanafunzi wa udaktari wanagharimiwa na Serikali kwa asilimia mia moja
wakati wanafunzi wenzao wa taaluma nyingine hawako hivyo.
Ndugu Wananchi;
Mwaka 2004/2005,
mshahara wa kuanzia wa daktari ulikuwa shilingi 178,700/=, mwaka 2005/ 2006
tuliupandisha na kuwa shilingi 403,120/=. Tuliendelea kuupandisha mwaka hadi
mwaka mpaka kufikia shilingi 957,700/= wanazolipwa sasa. Kiasi hicho ni mara
mbili ya mishahara ya watumishi wa taaluma nyingine wenye shahada ya kwanza
wanaoanza kazi ambao kwa wastani hupata shilingi 446,100/=.
Tunafanya hivyo kwa
kutambua na kuthamini nafasi maalum ya madaktari katika jamii na ukweli kwamba
bado tunayo safari ndefu ya kuziba pengo la madaktari nchini. Lakini inaonekana
juhudi zetu zote hizo hazithaminiwi.
Ndugu Wananchi;
Sina budi kusisitiza
kwamba tunapofanya hivyo tunaongozwa na uwezo tulio nao wa kulipa. Kwa sasa
hatuwezi kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi
3,500,000/= na posho zote zile. Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza
kazi yatakuwa shilingi 7,700,000/=. Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si
vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama
walivyo madaktari.
Kutokana na ukweli huo
basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya
kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa
muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana
sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa
mshahara huo. Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri
ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka. Huna sababu ya kumpa usumbufu
mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate
usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa
kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24.
Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa
hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na sheria za kazi na
maadili ya kazi ya udaktari.
Mamlaka za ajira
zimeanza kuchukua hatua hizo na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea
kugoma. Najua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa.
Hivyo, mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari
aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo
pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi. Vinginevyo atakuwa anajidanganya
kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuwathibitishia
kwamba dhamira ya Serikali ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wakiwemo
madaktari iko wazi. Tumekuwa tunafanya hivyo, na tutaendelea kufanya hivyo
kulingana na uwezo wa kibajeti. Ni vyema watumishi wa umma wakatambua kuwa
hatuwezi kutumia fedha zote au kiasi kikubwa mno cha pesa za umma kulipana
mishahara.
Tukifanya hivyo, Serikali itashindwa kutoa huduma muhimu kwa wananchi ambao ndiyo wengi na wanastahili kuhudumiwa. Hata hizo huduma za afya tunazosema ni duni tuziboreshe, hatutaweza kuziboreshakama
tutatumia sehemu kubwa ya pesa za Serikali kuwalipa mishahara wafanyakazi.
Tukifanya hivyo, Serikali itashindwa kutoa huduma muhimu kwa wananchi ambao ndiyo wengi na wanastahili kuhudumiwa. Hata hizo huduma za afya tunazosema ni duni tuziboreshe, hatutaweza kuziboresha
Hivi sasa matumizi ya
mishahara ni asilimia 48 ya bajeti ya Serikali. Kiwango hicho ni kikubwa
mno.
Uwiano mzuri ni kuwa na matumizi ya mishahara yasiyozidi asilimia 35 ya bajeti na asilimia 65 zitumike kugharimia huduma na shughuli nyingine za maendeleo ya wananchi na taifa. Sisi tumezidi kwa asilimia 13. Hivyo, hatuna budi tukubali kujinyima kwa manufaa ya walio wengi.
Uwiano mzuri ni kuwa na matumizi ya mishahara yasiyozidi asilimia 35 ya bajeti na asilimia 65 zitumike kugharimia huduma na shughuli nyingine za maendeleo ya wananchi na taifa. Sisi tumezidi kwa asilimia 13. Hivyo, hatuna budi tukubali kujinyima kwa manufaa ya walio wengi.
Suala la Dkt. Steven
Ulimboka:Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba
yangu, napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu
makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Steven
Ulimboka usiku wa tarehe 26 Juni, 2012. Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila
na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu
vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema
kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana
shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.
Natambua kuwa Serikali
nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani
siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa kiungo
muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na Madkatari. Ni kweli kwamba yeye
si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya.
Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari
wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa
na Serikali.
Ndugu Wananchi;
Ndugu Wananchi;
Kwa niaba yangu na kwa
niaba ya Serikali natoa mkono wa pole kwa Dkt. Steven Ulimboka na kumuombea
apone haraka ili aungane na familia yake na Watanzania wenzake katika ujenzi wa
taifa. Kwa namna ya pekee namshukuru na kumpongeza Bwana Juma Mgaza, kwa moyo
wake wa huruma na upendo na kwa hatua alizochukua za kumsaidia Dkt. Ulimboka.
Naomba kumaliza kwa
kuwasihi madaktari kuacha mgomo na kurejea kazini. Watanzania wenzenu
wanateseka na kupoteza maisha. Muwe na moyo wa huruma na upendo na msaada kwa
wagonjwa kama kiapo chenu kinavyowataka.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania !
Asanteni kwa
Kunisikiliza.
No comments:
Post a Comment