Mombasa Republican Council( MRC) ni vuguvugu lililoanzishwa
na wenyeji wa Pwani ya Kenya
wakitaka eneo hilo la Pwani lijitenge na Kenya na kuwa
nchi huru.
Mahakama imesema kuwa kundi hilo
ambalo makao yake makuu ni mjini Mombasa
sio kundi la kihalifu bali linaendesha harakati za kisiasa.
katika
uamuzi wake jopo la majaji watatu walishauri kundi hilo
kujisajili rasmi kama chama cha kisiasa.
Serikali
ilikipiga marufuku kikundi hicho cha MRC mwaka wa 2010, ikisema kuwa kundi hilo ni la kihalifu.
Lakini
Serikali imetangaza kuwa itakata rufaa kupinga uamuzi huo likidai kuwa ni
kinyume na katiba ya Kenya .
Wadadisi
wa maswala ya kisiasa wanasema kuwa uamuzi huo wa mahakama utalipa kundi hilo nguvu ya kuendeleza harakati zake za kutaka kujitenga
kutoka Kenya .
Kuna
hofu kuwa hali hii itatatiza uthabiti wa kisiasa nchini Kenya .
Kundi
hilo la MRC limekuwa likiilaumu serikali kwa
madai ya kuwa nyanyasa wakaazi wa pwani na kulitelekeza jimbo hilo zima.
Wakuu
wa MRC pia wamekuwa wakisema hawaoni faida kutokana na rasilmali zilizoko
pwani.
Kutokana
na harakati zao wasuasi wengi wa MRC wamekuwa wakikawatwa na kushitakiwa kwa
kuwa wanachama wa kundi haramu.
Baada
ya mahakama kutoa uamuzi wa kulindolea kundi hilo
marufuku iliyowekwa na serikali , sasa haijulikani kama
serikali itaondoa kesi za watu walioshitakiwa.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment