Afisa mmoja wa ngazi ya juu nchini Marekani ameonya kuwa
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, huenda akafunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita
kwa kuhusika na vita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .
Stephen Rapp, ambae ni mkuu wa kitengo cha jinai ya kimataifa
nchini Marekani, amesema hii inatokana na madai kuwa Rwanda
inawafadhili waasi wanaopigana katika mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo .
Afisa huyo amesema kuwa Rais Kagame huenda
akashtakiwa katika mahakama ya jinai ya kimataifa katika The Hague kwa madai ya
kuwafadhili waasi.
Ripoti
ya hivi majuzi ya Umoja wa mataifa juu ya mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Congo iliituhumu Rwanda kwa kuyawapa silaha makundi
ya waasi.
Hata
hivyo Rais Paul Kagame mwenyew amekanusha mara kadhaa kwamba serikali yake ina
husika kivyovyote na hita hivyo vya Congo .
Kagame
amepuuza habari hizi akisema kwamba maoni yao
hayakujumuishwa na walioandika ripoti hizo za kuwalaumu.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment