Ndugu zangu
Hakuna kazi ngumu kama ya uandishi wa habari hasa kitengo cha kupiga picha, leo nilikwenda kuchunguza kitu katika soko la samaki ferry, lakini katika harakati za kuwatafutia zawadi wanakijiji wenzangu humu bloguni nikataka kupiga picha ya wavuvi.
Jamaa wakaja juu kweli, wakataka kunipokonya kamera yangu na kunitosa baharini ili kuzima hasira zao. Bahati nzuri Mungu amenijaalia hekima na busara nikawabembeleza na wakanielewa.
Kosa nililofanya baada ya kuhisi wamenielewa nikaendelea kuwauliza 'sasa niwapige picha?' wakanitukana na kuniambia niondoke haraka sana kabla hawajanitosa baharini.
Jamani laiti ningekuwa Mzungu nataka kuwapiga picha wangenifukuza kama walivyofanya? Tuachane na hayo, baada ya hapo nilipokuwa nataka kupanda daladala kivukoni nikaamua kujifariji na hiyo picha ya muuza samaki aliechoka.
HAFIDH KIDO
0713 593894/ 0752 593894
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment