Watu wapatao 35 wamekufa kufuatia mafuriko yaliyotokea
katikati mwa Nigeria
baada ya mvua kubwa na kusababisha bwawa kufurika karibu na mji wa Jos.
Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu katika eneo hilo amesema nyumba
zipatazo 200, nyingi zikiwa zimejengwa kwa udongo zimezama au kuharibiwa na
mafuriko.
Maafisa wanasema watu wapatao ishirini na
watano hawajulikani walipo na kwamba idadi ya watu waliokufa inatarajiwa
kuongezeka.
Shirika
la Taifa la Kushughulikia Majanga limeanza operesheni ya misaada ya dharura.
Mtu
mmoja alinukuliwa akisema kuwa amewapoteza watoto wake saba katika mkasa huo.
Msemaji
wa shirika la msalaba mwekundu katika Jimbo la Plateau amesema miongoni mwa
waliofariki ni mzee wa miaka 90.
Chanzo:BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment