Mwishoni mwa wiki maelfu ya watu walijitokeza kando ya mto Thames mjini London kwa tamasha kubwa zaidi la BT River of Music, Nchi zote zinazoshiriki kwenye michezo ya Olimpiki ziliwakilishwa hapa. Mwanamuziki Angelique Kidjo, kutoka Benin, mi mmoja wa wasanii waliovutia umati mkubwa wa watu.
Gwiji wa muziki wa Jazz ambaye hucheza tarumbeta Hugh Masekela pia alikuwepo. " Mimi hujivunia kupiga muziki mzuri tu hasa nikiwa na wasanii wengine. Angelique Kidjo ni rafiki wangu mkubwa na anajua sana kuwatumbuiza watu." alisema Masekela kutoka Afrika Kusini.
Kwaya ya SAfricanto nayo iliwaleta pamoja waimbaji kutoka Botswana, Lesotho, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland na Zambia. Kwaya iliongozwa na mwimbaji wa Afrika kusini ambaye huimba Soprano Joyce Moholoagae (Kushoto).
Concha Buika aliwakilisha nchi ya wazazi wake, Equatorial Guinea, nchi pekee barani Afrika ambako wanazungumza kihispania. Alizaliwa mjini Mallorca, Uhispania na yeye huchanganya muziki wake wa flamenco na muziki wa kitamaduni wa hispania,coplas, rumba, soul, jazz na miondoko ya kiafrika.
Watu wengi pia walifurahia sana kumuona gwiji mwingine wa muziki kutoka Nigeria, King Sunny Ade ambaye hakuwa amepiga muziki wange mjini London kwa miaka mingi. Aliambia BBC kuwa anajiandaa kutoa album yake ambayo ataichanganyia London.
Mmoja wa manamuziki waliosubiriwa sana kwa hamu ni Baaba Maal, kutoka Senegal.
"Nafikiri London ilifanya vizuri sana kuleta pamoja tamaduni mbali mbali karibu na michezo. Ni sehemu mbili muhimu za maisha." Alisema Baaba Maal
No comments:
Post a Comment