Siku chache baada ya Rais mpya wa Misri
Mohammed Mursi kupuuza amri ya mahakama kuvunja Bunge iliyotolewa na baraza kuu
la kijeshi mahakama ya juu imepangua mchakato huo.
Wabunge walikutana kwa muda mfupi kabla ya
mahakama ya juu zaidi kutoa agizo lake
jipya .
Na
maelfu wa watu wamekusanyika katika medani ya Taharir kupinga uamuzi wa
mahakama hiyo ya juu.
Waandamanaji
wamekuwa wakipiga kelele wakisema hatua hiyo ni haramu na pia kulilaani baraza
la kijeshi la Misri.
Mwandishi
wa BBC mjini Cairo Jon Leyne anasema kuamuzi wa mahakama hiyo umeleta hali ya
utata kuhusu ni nani hasa ana uwezo na majukumu ambayo kawaida hutekelezwa na
bunge la nchi.
Kuna
dalili kwamba kitakachofuata sasa ni vita vya kisheria vya muda mrefu kuhusu
nani mwenye mamlaka halisi.
Kwa
sasa huenda rais na jeshi wakjaanza kushindani kila mmoja aktika kuonyesha kuwa
na uwezo zaidi.
Na
kuna hofu kuwa maandamano huenda yakaanza tena nchini Misri.
Katika
bunge ambalo Mahakama ya juu zaidi ili agiza livyunjwe wengi ya wabunge
walikuwa ni wanachama wa Muslim Brotherhood.
Siku
ya Jumanne wabunge waliitikia amri ya Rais Mursi na kukutana kwa muda mfupi
kabla ya vikao vyake kuhairishwa tena na Spika Saada al-Katatni.
Chanzo:
BBC swahili

No comments:
Post a Comment