Sunday, July 8, 2012

Makamu wa rais wa Afrika ya Kusini Kgalema Motlanthe, afanya ziara ya kimaendeleo Tanzania.


   
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk Mohammed G. Bilal, akimpokea Makamu wa Rais wa Afrika ya Kusini Kgalema Motlanthe, uwanja wa ndege wa JK Nyerere leo. Motlanthe, atakuwa Tanzania katikaziara ya siku mbili ambapo kesho atakuwa na mazungumzo na Makamu wa Rais wa Tanzania halafu keshokutwa atatembelea shule ya ANC iliyo Mkoani morogoro eneo la mazimbu.

Itakumbukwa wapiganaji wa kiafrika kutoka chama cha siasa cha ANC cha Afrika ya kusini kiliweka kambi yake mkoani Morogoro wakati wa kipindi cha vita ya ukombozi dhidi ya unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi miaka ya sabini na thamanini mpaka kupata uhuru wao kamili mwaka 1994.

No comments:

Post a Comment