Jeshi la Polisi Zanzibar
limelazimika kutumia Mabomu ya Machozi ili kuwatawanya wafuasi wa kikundi cha
Uamsho waliokuwa wamekusanyika kufanya Dua ya kuwaombea watu waliokufa katika
ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv. Skagit katika Mitaa ya Mbuyuni.
Habari kutokaZanzibar zinadai kuwa Jeshi hilo la Polisi
lililazimika kutumia Mabomu ya Machozi kutokana na kikundi hicho cha Uamsho
kuanza kuhubiri siasa badala ya kufanya Dua hatua iliyosabaisha kuvunjika kwa
amani katika mitaa hiyo.
Mwandishi wa Kituo hiki cha Uhuru FM aliyeko MjiniZanzibar amesema licha ya Watanzania
kuendelea kuomboleza vifo vya watu waliokufa katika ajali hiyo, bado kikundi
hicho cha Uamusho kimeendelea kufanya sisasa badala ya kufanya Dua.
Pia imeelezwa kuwa chanzo cha Mabomu hayo ya Machozi ni kikundi hicho kufanya Dua yenye utata huku masuala ya siasa yakijitokeza hatua iliyopelekea kuwepo kwa vurugu za hapa na pale hivyo Jeshi likaamua kutumia nguvu ya ziada ili kuwatawanya.
CHANZO: Radio Uhuru FM
Habari kutoka
Mwandishi wa Kituo hiki cha Uhuru FM aliyeko Mjini
Pia imeelezwa kuwa chanzo cha Mabomu hayo ya Machozi ni kikundi hicho kufanya Dua yenye utata huku masuala ya siasa yakijitokeza hatua iliyopelekea kuwepo kwa vurugu za hapa na pale hivyo Jeshi likaamua kutumia nguvu ya ziada ili kuwatawanya.
CHANZO: Radio Uhuru FM

No comments:
Post a Comment