Umoja wa nchi za Ulaya itaondoa vikwazo dhidi ya Zimbabwe mara
tu nchi hiyo itakapoanda kura ya maoni iliyo huru na ya wazi kuhusu katiba yake
mpya.
Mawaziri wa mambo ya nje wa umoja huo wamesema kuwa katiba
nzuri na inayokubalika na raia wengi ni hatua muhimu kwa nchi hiyo kuandaa
uchaguzi huru na wa haki.
Katika taarifa yao mawaziri hayo wamewaondolea vikwazo zaidi
ya wapambe 100 wa rais Robert Mugabe.
Viongozi
zaidi ya 100 wa Zimbabwe
akiwemo Rais Mugabe mwenyewe waliwekewa vikwazo tangu mwaka 2002 vikiwemo
kupigwa marufuku kusafiri nchi za Ulaya.
Lakini
William Hague,waziri wa Maswala ya njee wa Uingereza amesema kuwa Rais Mugabe
hakuondolewa vikwazo.
Vikwazo
hivyo vilivyoweka zaidi ya muongo mmjoja uliopita yalifuatia madai ya Zimbabwe
kukiuka haki za kibinadamu ikiwemo kuwa dhulumu na kuwanyanyasa upinzani.
Rais
Mugabe na mpinzani wake Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai, wamekuwa katika serikali
ya ugavi wa madaraka kufuatia utata uliokumba uchaguzi wa Zimbabwe wa
mwaka 2008.
Uchaguzi
mwengine unatarajiwa kuandaliwa mwaka ujao wa 2014 baada nchi hiyo ya kusini
mwa Afrika kupata katiba mpya.
Kwa
muda mrefu wapambe wa Rais Mugabe wamekuwa wakitaka vikwazo hivyo viongolewe
bila masharti yeyote wakidai kuwa vinaathiri uchumi wa Zimbabwe .
Nchi
hizo za Ulaya zilisema zinafurahishwa sana na
hatua ya nchi za SADC kutaka kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Zimbabwe .
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment