Monday, July 23, 2012

Wadau wa jembe mjini leo....

 huyu ni jembe wa Uhuru anaitwa Khamis. Hapa ni baada ya kutafuta habari na kufanikiwa kupata moja tu leo.
 Msafisha viatu vya waandishi maarufu mitaa ya Samora, anaitwa Lowassa huyu, muangalieni vizuri... ahahaa

 Jembe nami huwa sijitupi nikipata kijimiatano huwa nasafisha viatu vyangu. Naam umaridadi huficha umaskini, ingawa sox imetoboka...mhhhhhh.

 Huyu anaitwa Luis Columbia, nimetoka nae mbali sana huyu mtu. Tulikuwa pamoja katka uongozi wa TSJ na DSJ. Baadae tukapoteana na kuja kukutana The African New Habari. Na tukaopoteana tena kama miezi  mitatu, leo tumeonana tena mjini.

 Haya ni majembe nayo kwa mbaali namuona mwandishi wa Radio Quran, hapa mbele ni Mwinshehe wa Jambo leo, na Bukuku mmiliki wa www.fullshangwe.blogspot.com .

 Bakari kimwanga wa Mtanzania akiwa na wadau wake, Mwinshehe na Bukuku wakifurahia jambo.


 Huyu ni Imani Mwanahapa, leo nimepata bahati ya kukutana na wadau wangu niliopotezana nao siku nyingi. Ni mwandishi pia huyu tena mzuri alikwahi kuandikia The Guardian. Nilikuwa nae TSJ kwa Diploma, halafu nikakutana nae KIU- Kampala tukakaa kwa miaka mitatu mimi nikifanya shahada ya mawasiliano ya umma yeye akifanya shahada ya utalii. Tumepoteana kwa miezi takriban tisa, tangu tulipomaliza mitihani mwaka jana mwezi wa kumi na moja.

Huyu anaitwa Seif Oddo, akisalimiana na Kimwanga. Pia tulipoteana nae miaka mingi yapata miwili. Mimi na Seif pamoja na Kimwanga tulikuwa pamoja TSJ. Tena wakati huo mimi jembe lenu nikiwa Rais wa Chuo, Kimwanga waziri mkuu na Seif waziri wa Michezo na burudani.... Kwa sasa Seif yupo Sekta ya utalii kitengo cha habari, mimi na kimwanga tunagombana katika magazeti.

No comments:

Post a Comment