Timu ya mpira wa miguu ya
mkoani Mbeya Tukuyu Stars imeamua kurudi upya ili kuwapa burudani wapenzi wa
soka wa mkoa huo.
Akizungumza na wanahabari
katika ukumbi wa idara ya habari MAELEZO leo asubuhi msemaji wa timu hiyo
Kennedy Mwaisabula, amesema imefika wakati wameamua kuunda kamati maalum
itakayoirudisha timu hiyo katika ligi kuu ya Tanzania bara ili kurudisha ile
burudani iliyokosekana kwa kipindi kirefu.
Itakumbukwa Tukuyu Stars ni
miongoni mwa timu chache zisizozidi saba za Tanzania bara kuweza kunyakua
ushindi wa ligi kuu hapa nchini.
Timu hiyo ilipanda daraja
mwaka 1985 na kufanikiwa kuchukua ubingwa mwaka 1986, ni timu iliyoweka rekodi
ambayo haijawahi kuvunjwa mpaka sasa kwa kupanda daraja ndani ya mwaka mmoja na
kufanikiwa kuchukua ubingwa mwaka uliofuata.
Baadhi ya wachezaji waliowahi
kungara na timu hiyo ni Justin Nicodemus Mtekele (marehem), Aston Pardon,
Sekilojo Chambua, Hussein Zito, Stephen Mussa (Marehem), Jabir Mohamed
(Marehem), Peter Mwakibibi, Godwin Aswile (Scania), Salum Kabunda (Ninja), na
wengine wengi.
HAFIDH KIDO
0713 593894/ 0752 593894
DAR ES SALAAM , TANZANIA
<Kushoto kabisa alievaa shati la mistari ni mchezaji wa zamani wa Tukuyu Stars Godwin Aswile.
Jembe lililowahi kuchezea Tukuyu Stars, Simba na Timu ya Taifa Mosses Mkandawile (Golikipa)



No comments:
Post a Comment