Na hafidh Kido
Yanga ya jangwani leo
imefanikiwa kutinga fainali kwa mara nyingine baada ya kuitungua APR ya Rwanda kwa bao
moja mtungi katika dakika 30 za nyongeza, bao lililofungwa kiufundi na Hamis
Kiiza mnamo dakika ya 10 za mwanzo.
Yanga ambayo ina sifa ya
kuchukua kombe hilo mara nyingi kuliko klabu
yoyote hapa Tanzania ndiyo
mabingwa watetezi wa kombe la Kagame hivyo kutoa nafasi nzuri ya kulibakisha
nyumbani kombe hilo
linaloandaliwa na chama cha soka cha Afrika mashariki na Kati CECAFA
inayoongozwa na Rais wa TFF Leodger Ochila Tenga.
Hata hivyo mchezo wa leo
uliingia dosari kwa upande wa Yanga baada ya mchezaji wao Godfrey Taita kulamba
kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa APR mnamo dakika ya 14 ya
kipindi cha kwanza dakika za nyongeza; hivyo kuilazimu timu hiyo yenye makazi
yake mtaa wa twiga kucheza pungufu kwa dakika zote 15 zilizobakia.
Yanga itakutana na Azam FC
iliyoingia fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuichabanga bao
tatu moja bila huruma timu kongwe ya wekundu wa msimbazi Simba siku ya jumanne
katika uwanja wa taifa.
Fainali ya michuano hiyo
itachezwa jumamosi katika uwanja wa taifa ambapo imekuwa ni fahari kubwa kwa
mashabiki wa soka Tanzania
kwani kombe hilo litalazimika kubaki katika
ardhi hii iwe isiwe kwa kuwa timu zinazochuana katika hatua ya mwisho ya
michuano hiyo zote ni za Tanzania .
HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM , TANZANIA
26/07/2012
0713 593894/ 0752 593894
No comments:
Post a Comment