Askofu mpya kabisa
kutawazwa imearifiwa kuwa anashikiliwa na mamlaka ya Uchina baada ya kutangaza
kuwa anajiuzulu kutoka Kanisa Katoliki linalokubalika na Mamlaka ya Uchina.
Thaddeus
Ma Daqin, Askofu wa Shanghai , alitangaza hatua
yake ya kujiuzulu kutoka Chama kijulikanacho kama
China Patriotic Association (CPA) siku ile ambapo alitawazwa wiki iliyopita.
Duru
za Kanisa Katolika na vyanzo vingine vya kidini vimesema kuwa kiongozi huyo wa
dini anashikiliwa ndani ya Seminariyo moja karibu na Shanghai .
Kwa
mda mrefu kumekuwepo hali ya kutofahamiana baina ya Uchina na Vatican .
Waumini
wanaokadiriwa kutimu milioni 10 wa huko Uchina wamegawika kati ya wafuasi wa
Papa na upande wa pili ukikubaliana na kundi la Chinese Patriotic Catholic
Association (CPA).
Taarifa
zinasema kuwa Askofu Ma aliuambia ummati wa watu 1,000 kuwa ameamua kujiuzulu
ili awezew kushughulikia majukumu yake mapya. Tangazo lake hilo
lilifuatiwa na makofi ya waumini , kwa mujibu wa habari za gazeti
linalochapishwa huko HongKong la South China Morning Post.
Lakini
wadadisi wanasema kuwa hatua hio ilionekana na wakuu wa Uchina kama kejeli na kudharau udhibiti wa Dola la Uchina juu ya
viongozi wa Kanisa Katoliki na wengine.
Chanzo: BBC swahili
<

No comments:
Post a Comment