Wednesday, July 4, 2012

Wandugu

wanakijiji wenzangu

Ile hali ya kusumbuliwa na mtandao wa internet ofisini leo imenisababishia sikuweza kuzungumza nanyi kwa siku yote ya leo.

Nilifika ofisini mapema, kama unavyofahamu leo ndiyo gazeti letu la Raia Mwema linatoka, tukajadili gazeti (post mo term) na kusubiri wakati wa kuwasiliana nanyi. Nilipojaribu kuanza kutuma picha na habari za leo nikaona mtandao una mafua (unasuasua), nikadhani ni tatizo la muda mdogo na litaisha.

Lakini kadiri muda ulivyosogea nikazidi kugundua tatizo ni la muda mrefu. Hatimae mpaka narudi nyumbani jioni hii sikuwa nimefanikiwa kutuma hata neno moja.

Bahati nzuri nilikuwa na hakiba yangu ya Tsh 1000 mfukoni nimenunua kifurushi cha Tsh 700, ndiyo imeweza kunipa uhai wa kuzungumza nanyi tena.


Nina picha nyingi, siwezi kuzituma zote, nitajaribu kutuma chache mafuta yatakapoishia nitamalizia kesho ofisini katika mtandao wa mserereko (bure). Naam bure siku zote ni ghali. Niombeeni nipate wadhamini mtafurahi.

HAFIDH KIDO

0752 593894/ 0713 593894
DAR ES SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment