Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, Hillary
Clinton, amekutana na viongozi wa Kenya katika sehemu ya mwisho ya
safari yake ya Afrika.
Hillary Clinton alifanya mazungumzo na Rais
Kibaki na Waziri MKuu Raila Odinga.
Bi
Clinton alisema mazungumzo yake yalihusu maswala kadha pamoja na uchaguzi wa
mwaka ujao nchini Kenya , na
hali katika nchi ya jirani, yaani Somalia ,
ambako wanajeshi wa Kenya
wanapigana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Al Shabaab.
Bibi
Clinton anaarifiwa kuiambia Kenya
kuwa Marekani iko tayari kuisaidia Kenya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka
ujao, na Marekani inataraji uchaguzi huo utafanywa kwa salama.
Bibi
Clinton piya alitarajiwa kukutana na wawakilishi wa serikali ya mpito ya Somalia walioko Nairobi .
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment