Mpatanishi wa Umoja wa Afrika, Thabo Mbeki, ametangaza
mapatano baina ya Sudan na Sdudan Kusini kuhusu malipo ya mapato ya mafuta
baada ya mzozo wa miezi kadhaa, ambao ulikaribia kuingiza mataifa hayo mawili
vitani.
Bwana Mbeki aliwaambia waandishi wa habari
katika mji mkuu wa Ethiopia ,
Addis Ababa ,
kwamba maswala yote yaliyokuwa yamebaki, sasa yametatuliwa, lakini hakutoa
maelezo zaidi.
Sudan
Kusini ilisitisha usafirishaji wa mafuta kupitia Sudan
mwezi wa Januari, kufuatia mzozo kuhusu ada iliyokuwa ikitozwa na serikali ya Khartoum .
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment