Sunday, August 12, 2012

Futari ya leo

Asalam,

Niwatake radhi kwa kuwakimbia kwa siku kadha, lakini jembe nilipatwa na msiba nikaenda Tanga kuzika. Namshukuru Mungu tumemaliza salama na sasa nimerejea mjini. Ingawa bado sijatulia niliacha viporo vingi vya kazi za gazetini na hata za Kidojembe.

Tatizosona msaidizi wa kuweza kumaliza baadhi ya mambo katika kidojembe, lakini nadhani leonitamtambulisha msaidizi wa Jembe kutoka Tanga. Si vibaya pia nikipata msaidizi wa Jembe kutoka Dar es Salaam, zipo taratibu za kufuata na akama utaridhika unaweza kuwasiliana nami kupitia namba zangu za simu. VIGEZO NA MASHARTI, KUZINGATIWA.

Leo tutafuturu Tambi za mchele na nazi, vibibi, muhogo na uono (dagaa mchele) wa kukaanga. Halafu tutakuwa na matunda kama kawaida yetu na maji meengi.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894, 0752 593894
13, AUGUST, 2012


No comments:

Post a Comment