Asalam allaykum,
poleni ndugu zangu leonimechelewa sana kuwasiliana na nyinyi kwa maana nilipitiwa na kausingizi ka sikukuu. Si unajua leo wakulima wanasherehekea siku yao. Naam tarehe nane mwezi wa nane ni sikukuu ya wakulima.
Futari yteu ya leo itakuwa kalmati za sukari nje, kunde za sukari, majimbi ya nazi, samaki wa kukaanga, chapati na mchuzi wa maini. Uji wa unga wa muhogo uliotiwa pilipili manga (black pepper) na juice ya machungwa.
No comments:
Post a Comment