Na Danstan Shekidele
Siku chache kabla ya
kifo chake askari polisi mwenye namba F 3276, Donald Mathew (33), aliyejinyonga
juu ya mti katika daraja la Shani, mkoani Morogoro alimwandikia barua Waziri wa
Mambo ya Ndani kueleza kinachodaiwa kuwa ni ufisadi unaofanywa na vigogo wa
polisi nchini, imebainika.
Polisi huyo
aliyefahamika sana
kwa jina la Dunga aliwahi kutoa tuhuma nzito dhidi ya maofisa, wakaguzi na
polisi wa kawaida, mkoani Morogoro mwaka jana lakini hakuna hatua
zilizochukuliwa dhidi ya maofisa hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Morogoro, Fustine Shilogile, jana alisema jeshi hilo , lilipokea taarifa za kujinyonga Mathew
jana asubuhi.
Alisema askari huyo,
aijinyonga kwa kutumia vipande vya kamba ya kanga ambavyo viliunganishwa na
hakuacha ujumbe wowote unaoeleza sababu ya kuchukua uwamuzi huo.
Alisema askari huyo
kabla ya kufanya tukio hilo ,
alionekana mitaani akinywa pombe katika Baa ya Shani.
Alisema baada ya
kuonekana amelewa, Mathew aliamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu, kitendo
kilichofanya baadhi ya askari polisi waliokuwa eneo hilo , kumfuata na kumsihi avae nguo.
Alisema marehemu,
alihamishiwa mkoani Singida kikazi, lakini Novemba, mwaka jana aliamua kuacha
jeshi.
“Pamoja na kwamba
marehemu aliacha kazi mwaka jana, sisi kama jeshi bado tunamtambua kama askari mwenzetu… kwa msingi huo tutasafirisha mwili
wake Agosti 8, mwaka huu kwenda nyumbani kwake mkoani Kilimanjaro,” alisema
Kamanda Shilogile.
Alipoulizwa kama kifo
cha Mathew kimesababishwa na baadhi ya askari waliohusishwa kwenye tuhuma za
kuhusika na biashara za dawa za kulevya, Kamanda Shilogile alisema uchunguzi
unaendelea, na kwamba ikibainika kama kuna
askari aliyehusika atachukuliwa hatua kali.
Hata hivyo, askari huyo
mwishoni mwa mwaka jana, alitoa tuhuma mbalimbali ambazo zilichapishwa katika
moja ya magazeti linalotoka mara mbili kwa wiki, zikiwatuhumu askari 9 wa
kikosi cha kupambana na majambazi wa kutumia silaha kupokea rushwa kutoka kwa
wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
Tuhuma nyingine alizotoa
ni polisi kukamata majambazi wenye silaha, lakini huachiwa baada ya kupewa
fedha na mali
mbalimbali, hivyo kushindwa kuwafikisha kituoni.
Alisema tuhuma nyingine
ni polisi kuwakamata wafanyabiashara wa pombe haramu aina ya gongo na bangi
bila kuwachukulia hatua zozote baada ya kuhongwa.
Tuhuma nyingine,
zinazodaiwa kufanywa na askari hao ni kushirikiana na matapeli, kutapeli raia
wa kigeni na kushirikiana na majambazi kuvunja maduka na kuiba mali za
wafanyabiashara nyakati za usiku
Chanzo Mjengwablogspo
No comments:
Post a Comment